Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rombo wamepatiwa elimu kuhusu ugonjwa wa Monkeypox (MPOX) katika semina maalumu iliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rombo.
Semina hiyo imehudhuriwa na wataalamu wa afya kutoka wilaya ya Rombo na kuelimishwa kuhusu dalili za ugonjwa wa MPOX, njia za maambukizi, na mbinu za kujikinga na ugonjwa huo ili wawe mabalozi katika jamii inayowazunguka.
Aidha watumishi hao wamehimizwa kuchukua tahadhari kwa kufuata kanuni za usafi wa mwili kama unawaji wa mikono mara kwa mara pia matumizi sahihi ya barakoa ili kupunguza hatari ya maambukizi katika wilaya hiyo.
Rombo District Council,Mkuu Bomani Street
Sanduku la Posta: P.o Box 52,Mkuu,Rombo
Simu: 027-2757101
Simu ya Mkononi: 027-2757101
Barua Pepe: ded@rombodc.go.tz
Copyright@2019Rombodc.all rights reserved