HALMASHAURI YA WILAYA YA ROMBO
Orodha ya miradi ya Maendeleo inayoendelea na iliyosimama kutekelezwa
| Na | Aina ya mradi | Sekta | Mahali ulipo | Hatua ya utekelezaji | 
| 1 | Ujenzi wa jengo la Utawala (HQ) | Utawala | Bomani | Msingi | 
| 2 | Mradi wa   maji kijiji cha Shimbi Mashariki | Maji | Shimbi mashariki | Utekelezaji unaendelea | 
| 3 | Mradi wa  maji Kijiji cha Ngareni | Maji | Ngareni | Utekelezaji unaendelea | 
| 4 | Mradi wa  maji Kijiji cha Ushiri | Maji | Ushiri | Umekamilika | 
| 5 | Mradi wa  maji Kijiji cha Kahe | Maji | Kahe | Umekamilika | 
| 6 | Mradi wa maji Kijiji cha Leto | Maji | Leto | Utekelezaji unaendelea | 
| 7 | Ujenzi wa OPD awamu ya II katika kituo cha Afya Karume | Afya | Lesoroma | Msingi | 
| 8 | Ukarabati wa Ofisi ya Idara ya Ardhi | Utawala | Bomani | Jengo limepauliwa | 
| 9 | Ukarabati wa machinjio Kijiji cha Ibukoni | Mifugo | Ibukoni | Uchakavu wa miundombinu | 
| 10 | Kukamilisha Ujenzi wa Ofisi ya Kero | Utawala | Bomani | Jengo limeshapauliwa (Awamu ya I imekamilika) | 
| 11 | Ujenzi wa nyumba ya mtumishi awamu ya II-Mkuu mjini | Utawala | Mkuu mjini | Jengo lishapauliwa (Awamu ya I imekamilika) | 
| 12 | Ujenzi wa matenki 5 ya kuvunia maji ya mvua katika shule ya msingi Baraka, Kwalamtongi, Keni Aleni, shule ya sekondari Kilamacho na Zahanati ya Ikuini | Maji | Kirongo juu,Marangu,Aleni chini, Kiraeni na Ikuini | Utekelezaji unaendelea na Ujenzi upo katika hatua mbalimbali | 
| 13 | Ujenzi wa uzio (gate),mfumo wa kutolea taka soko la Mkuu | Kilimo | Mkuu | Uchakavu wa miundombinu | 
| 14 | Ukamilishaji wa kitalu cha miche ya kahawa ya vikonyo katika Kijiji cha Samanga | Kilimo | Samanga | Ujenzi wa uzio na ununuzi wa vifaa vya ujenzi wa machipuzo (VPU) | 
| 15 | Ujenzi wa Bweni la Wavulana katika Shule ya Sekondari Mahida | Elimu | Mahida | Jengo limepauliwa, bado umaliziaji | 
| 16 | Ujenzi wa vyoo katika Shule ya Msingi Kikelelwa, Mokombero, Mahorosha na Malowa | Elimu | Kikelelwa,Mokombero,Mahorosha na Kidondoni | Kikelelwa Ujenzi wa choo umekamilika na kinatumika. Mokombero choo cha dharura matundu 4 kimechimbwa Mahorosha shimo la choo limechibwa Malowa choo kimepauliwa | 
| 17 | Ujenzi wa Ofisi ya vijiji katika kijiji cha Samanga | Utawala | Samanga | Ujenzi upo katika hatua za mwisho za umaliziaji | 
| 18 | Upandaji wa miche ya miti 300,000 kwenye msitu wa Half Mile | Misitu | Nusu maili | Miti 215,000 imepandwa katika msitu wa nusu maili | 
| 19 | Ukamilishaji wa soko la Holili | Kilimo | Holili | Awamu ya I imekamilika | 
| 20 | Ukamilishaji wa Nyumba moja ya mtumishi katika Zahanati ya Kirongo Chini | Afya | Kirongo chini | Ujenzi wa boma umekamilika | 
| 21 | Ukamilishaji wa Nyumba ya Mtumishi katika Zahanati ya Mengeni Kitasha | Afya | Kitasha | Hatua za mwisho za umaliziaji | 
| 22 | Ukamilishaji wa ujenzi wa Zahanati ya Ngaseni | Afya | Ngaseni | Hatua ya Lenta na Ujenzi unaendelea | 
| 23 | Ukamilishaji wa ujenzi wa Zahanati ya Kisale | Afya | Kisale | Ujenzi wa boma umekamilika na unaendelea | 
| 24 | Ujenzi wa ofisi ya Kijiji cha Nguduni | Utawala | Mahida - Nguduni | Jengo lipo hatua ya usawa wa dirisha na Ujenzi umesimama | 
| 25 | Ujenzi wa Zahanati ya mawanda mkei | Afya | Mahida - Mahango | Eneo lipo, mawe na mchanga na utekelezaji unaendelea | 
| 26 | Ujenzi wa madarasa 8 shule ya msingi Kastam | Elimu | Holili | Madarasa yamepauliwa na Ujenzi unaendelea | 
| 27 | Ujenzi wa ofisi ya Kijiji Mamsera Kati | Utawala | Mamsera Kati | Jengo limepauliwa na Ujenzi unaendelea | 
| 28 | Ujenzi wa darasa la awali Kijiji cha Kidondoni | Elimu | Chala - Kidondoni | Ujenzi umefikia hatua ya Lenta na Ujenzi umesimama | 
| 29 | Ujenzi wa ofisi ya Kijiji cha Mengwe Juu | Utawala | Mengwe Juu | Jengo limepauliwa na Ujenzi unaendelea | 
| 30 | Ujenzi wa ofisi ya Kata ya Manda | Utawala | Manda – Manda Chini | Jengo limepauliwa na Ujenzi unaendelea | 
| 31 | Ujenzi wa choo cha kisasa shule ya msingi Ngoyoni | Elimu | Ngoyoni – Ngareni | Shimo limechimbwa na utekelezaji unaendelea na utekelezaji unaendelea | 
| 32 | Ujenzi wa ofisi ya Kata Ngoyoni | Utawala | Ngoyoni | Jengo limepauliwa na Ujenzi umesimama | 
| 33 | Ujenzi wa maabara shule ya Sekondari Mengeni | Elimu | Mengeni – Mengeni Chini | Jengo limepauliwa na kuwekwa meza na utekelezaji unaendelea | 
| 34 | Ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Mfuruwashe | Afya | Mengeni - Mfuruwashe | Ujenzi upo katika hatua ya msingi | 
| 35 | Ujenzi wa darasa la awali shule ya msingi Kwasondo | Elimu | Shimbi masho | Jengo limepauliwa, vioo vimewekwa sakafu na plasta na linatumika | 
| 36 | Ujenzi wa madarasa 3 shule ya Sekondari Kwaikuru | Elimu | Shimbi – Mashami | Madarasa yamepauliwa | 
| 37 | Ujenzi wa darasa 1 shule ya sekondari Mlambai | Elimu | Shimbi kwandele | Ujenzi umefikia hatua ya lenta | 
| 38 | Ujenzi wa madarasa 2 shule ya sekondari Makiidi | Elimu | Makiidi - Maharo | Madarasa yamepauliwa na yanatumika ila bado hayajakamilika | 
| 39 | Ujenzi wa Zahanati kijiji cha Ubaa | Afya | Ubaa | Hatua ya kuchimba msingi | 
| 40 | Ujenzi wa ofisi ya Kata ya Mrao Keryo | Utawala | Mrao Keryo | Ujenzi umefikia hatua ya lenta | 
| 41 | Ujenzi wa Zahanati kijiji cha Keryo | Afya | Keryo | Ujenzi umefikia hatua ya kuweka lenta na utekelezaji unaendelea | 
| 42 | Ujenzi wa ofisi ya kijiji cha mrere | Utawala | Katangara mrere | Ujenzi upo katika hatua ya lenta | 
| 43 | Ujenzi wa Zahanati ya kijiji cha Kisale | Afya | Kisale | Ujenzi upo katika hatua ya boma na utekelezaji unaendelea | 
| 44 | Ujenzi wa wodi ya Zahanati ya Mahorosha | Afya | Mahorosha | Ujenzi upo katika hatua ya msingi | 
| 45 | Ujenzi wa ofisi ya kijiji cha Marangu | Utawala | Marangu | Ujenzi upo katika hatua ya mwisho ya umaliziaji | 
| 46 | Ukarabati wa madarasa 3 shule ya msingi Baraka | Elimu | Kirongo juu | Madarasa hayana madirisha, milango, plasta na sakafu imeharibika | 
| 47 | Ujenzi wa madarasa 2 shule ya msingi Kiraro | Elimu | Lesoroma | Madarasa yamepauliwa na utekelezaji unaendelea | 
| 48 | Ukarabati wa madarasa 4 shule ya msingi Usongo | Elimu | Kingachi - Leto | Utekelezaji unaendelea | 
| 49 | Ukarabati wa madarasa shule ya sekondari Nanjara | Elimu | Nanjara | Uchakavu wa miundombinu | 
| 50 | Ujenzi wa ukumbi wa mitihani shule ya sekondari Urauri | Elimu | Urauri | Ujenzi umefikia hatua ya lenta | 
| 51 | Ujenzi wa ofisi ya kata ya Reha | Utawala | Reha - Nesae | Jengo limepauliwa na kuwekwa  milango | 
| 52 | Ujenzi wa nyumba ya mganga Zahanati ya Kikelelwa | Afya | Kikelelwa | Nyumba imepauliwa na utekelezaji umesimama | 
| 53 | Ujenzi wa Zahanati ya kijiji cha Nduweni | Afya | Mbomai | Ujenzi umefikia hatua ya lenta | 
| 54 | Ukarabati wa madarasa 3 na Ujenzi wa darasa la awali shule ya msingi Endoneti | Elimu | Endoneti | Utekelezaji unaendelea | 
| 55 | Ujenzi wa jiko la kisasa shule ya msingi Kwangao | Elimu | Kelamfua | Awamu ya I Ujenzi imekamilika | 
| 56 | Ujenzi wa jiko shule ya Sekondari Horombo | Elimu | Ibukoni | Jiko na stoo zimejengwa bado Ujenzi wa bwalo | 
| 57 | Ujenzi wa Ofisi ya Kijiji cha Kidondoni | Utawala | Kidondoni | Ujenzi umekamilika | 
| 58 | Ujenzi wa jengo la Zahanati Kijiji cha Kiraeni | Afya | Kiraeni | Ujenzi upo katika hatua za awali | 
| 59 | Ujenzi wa Kituo cha Polisi  Kirongo chini | Utawala | Kirongo chini | Ujenzi umefikia hatua ya lenta na utekelezaji umesimama | 
| 60 | Ujenzi wa Kituo cha Polisi  Ngoyoni | Utawala | Ngoyoni | Ujenzi upo katika hatua ya lenta | 
 
                              
                              
                            Rombo District Council,Mkuu Bomani Street
Sanduku la Posta: P.o Box 52,Mkuu,Rombo
Simu: 027-2757101
Simu ya Mkononi: 027-2757101
Barua Pepe: ded@rombodc.go.tz
Copyright@2019Rombodc.all rights reserved