Kutoa ushauri wa kilimo cha mazao mbalimbali kupitia Maafisa Ugani walioko katika ngazi za vijiji na wilaya ili wakulima waweze kuzalisha kwa tija.
Maafisa Ugani wamekuwa wakitoa elimu ya uzalishaji mazao kwa kutumia njia mbalimbali kama vile:- Mashamba darasa, vishamba vya mfano(Demo plots), vikundi vya wakulima pamoja na kuwatembelea wakulima mmoja mmoja shambani kwake (Farm &Home Visit)
Kusimamia kilimo kinachozingatia hifadhi ya ardhi na mazingira kwa kuwapimia wakulima Makinga maji ili kuzuia mmomonyoko wa ardhi pamoja na kuvuna maji ya mvua yanayotiririka barabarani na kuyaingiza mashambani.
Kuunganisha wakulima na Masoko ya mazao mbalimbali ndani na nje ya wilaya.
Kuhakikisha upatikanaji wa pembejeo bora za kilimo na kwa wakati.
Kuelimisha wakulima juu ya Hifadhi bora ya mazao baada ya kuvuna.
Kusambaza teknolojia mpya kutoka katika vituo vya utafiti na kuzifikisha kwa wakulima kwa ajili ya utekelezaji.
Kutoa elimu kwa wauza pembejeo ili wanunue pembejeo bora zinazoendana na mazingira ya wilaya ya Rombo