PROFAILI YA IDARA YA USAFI NA MAZINGIRA
|
Dira yetu; Watu wenye afya katika mazingira mazuri na endelevu.
Mission yetu; Inalinda afya za watu kutokana na hatari za kimazingira.
Utangulizi.
Idara ya Usafi na Mazingira inaye Mkuu wa Idara, Afisa Afya Mazingira 1, Maafisa afya Mazingira wasaidizi 12,Wasaidizi wa afya mazingira 4, mbapo kata zenye wataalamu ziko 14 tu kati ya kata 28, upungufu uliopo ni maafisa afya Mazingira wasaidizi 14.
Moja ya majukumu ya Sekta ya Usafi na Afya Mazingira ni kudhibiti mazingira anayoishi binadamu , kufanya kazi na kupita ili mazingira hayo yasiwe chanzo cha magonjwa mbalimbali ya kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza kwa binadamu.
Shughuli za Usafi na Afya Mazingira zinaongozwa na kuongozwa chini ya Sheria mbalimbali zilizotungwa na bunge zikiwemo; Sheria namba 1 ya Afya ya jamii ya mwaka 2009 pamoja na kanuni zake za mwaka 2016 zilizochapishwa katika Gazzeti la Serikali namba 226 la tarehe 29.Juni.2012.
Sheria namaba 1 ya Chakula,Dawa na Vipodozi ya mwaka 2003 pamoja na kanuni zake za mwaka 2006 zilizochapishwa katika Gazzeti la serikali namba 112 la tarehe 25.Agosti.2006.
Pamoja na Sheria ndogo za Halmashauri ya wilaya ya Rombo za mwaka 2017.
Baadhi ya majukumu yanayotekelezwa na idara hii ni;
Kufanya ufuaatiliaji wa utekelezaji wa kampeni ya kitaifa ya usafi wa mazingira (M&E) katika vijiji vyote 68 vilivyofikiwa wakati wa utekelezaji kuanzia ngazi ya kaya, kitongoji, kijiji na kata tangu mwaka 2013 hadi 2016, ili kuishawishi jamii iweze kuboresha hali ya usafi wa maingira ikiwa ni pamoja na ujenzi na matumizi ya vyoo bora pamoja na utengenezaji wa geleni/vifaa chirizi vya kunawia mikono na sabuni baada ya kutoka kujisaidia chooni.
Kusimamia na kuratibu kazi za uzoaji taka ngumu na laini katika miji na masoko katika masoko na stendi.
Kutekeleza,Kusimamia na kuratibu shughuli za ukaguzi wa maeneo ya kutengeneza na kuuzia vyakula na vinywaji ndani ya wilaya pamoja na kuchukua hatua za kisheria kwa wanaokiuka sheria na kanuni za afya mazingira
Kutekeleza,Kusimamia na kuratibu shughuli za ukaguzi wa maeneo ya taasisi,makazi,viwanda,karakana na maeneo yote anyopita,anayoishi ama kufanya kazi binadamu na kutoa ushauri ili maeneo hayo yasiwe chanzo cha magonjwa ama madhara kwa binadamu kwa mazingira yanayomzunguka binadamu.
Kufanya ukaguzi wa vyanzo vya maji na kutoa elimu ya afya na ushauri juu ya utunzaji wa vyanzo hivyo
Kushauri na Kuchukua hatua za kisheria kwa wale wote wanaoenda kinyume na sheria za nchi zinazohusiana na Usafi na Afya Mazingira.
Rombo District Council,Mkuu Bomani Street
Sanduku la Posta: P.o Box 52,Mkuu,Rombo
Simu: 027-2757101
Simu ya Mkononi: 027-2757101
Barua Pepe: ded@rombodc.go.tz
Copyright@2019Rombodc.all rights reserved