Wilaya kupitia Idara ya Elimu ina jukumu la kusimamia ubora wa utoaji wa Elimu kuanzia elimu ya Awali mpaka Sekondari yakiwemo mafunzo ya ufundi pamoja na yafuatayo:-
- Upanuzi wa elimu ya awali, msingi, sekondari, watu wazima na ufundi.
- Kuinua kiwango cha uandikishaji wanafunzi na kusimamia mahudhurio.
- Kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia.
- Kuratibu ujenzi wa miundombinu ya shule pamoja na upatikanaji wa samani.
- Kuratibu ununuzi wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia.
- Kuinua ubora na kiwango cha taaluma.
Elimu ya Awali
Halmashauri ya wilaya ya Rombo ina madarasa ya awali 159 kati ya hayo 151 yapo katika shule za serikali na 8 yapo katika shule za mashirika ya dini na watu binafsi. Shule moja ya walemavu haina darasa la awali.Madarasa hayo yako ndani ya shule za Msingi.
Elimu ya Msingi
Wilaya ya Rombo ina jumla ya shule 160 za msingi 152 za serikali na 8 za binafsi (kati ya shule za serikali moja ni ya walemavu.
Huduma zinazotolewa na Idara ya elimu msingi
Elimu Sekondari
Idara ya Elimu Sekondari inasimamia jumla ya shule za Sekondari 51. Kati ya hizo shule 41 ni za Serikali na 10 ni za Binafsi (Private Schools).
Shule za Serikali zina jumla ya wanafunzi 16,434 (ME= 6,800 na KE 9,634) na shule za Binafsi zina jumla ya wanafunzi 2,797 (ME= 1,216 na KE= 1,581). Hivyo jumla ya wanafunzi wote wa shule za Serikali na za Binafsi ni 19,231 (ME=8,016 na KE= 11,215).
Katika shule hizo 51 shule tano (5) zina wanafunzi wa Kidato cha Tano na Sita.zikiwemo 2 za Serikali na 3 za Binafsi.
Kuna jumla ya walimu 1,036 (ME= 584 na KE= 452). Data zote hizi ni kwa mujibu wa takwimu za tarehe 31 Machi,,29017.
Huduma zinazotolewa na Idara
Rombo District Council,Mkuu Bomani Street
Sanduku la Posta: P.o Box 52,Mkuu,Rombo
Simu: 027-2757101
Simu ya Mkononi: 027-2757101
Barua Pepe: ded@rombodc.go.tz
Copyright@2019Rombodc.all rights reserved