Eneo na Mipaka
Halmashauri ya Wilaya ya Rombo ni miongoni mwa Halmashauri sita (6) na Manispaa moja (1) zinazounda Mkoa wa Kilimanjaro ambazo ni; Hai, Same, Mwanga, Moshi, Siha na Manispaa ya Moshi.Wilaya hii ilianzishwa mwaka 1972.
Eneo la Wilaya ni kilomita za mraba 1,442 sawa na Hekta 144,000. Wilaya inapakana na nchi ya Kenya kwa upande wa Kaskazini na Mashariki. Upande wa Kusini na Kusini-Magharibi inapakana na Wilaya ya Moshi, Kaskazini-Magharibi inapakana na Wilaya za Siha na Longido iliyoko Mkoa wa Arusha.
Matumizi ya Ardhi
Hekta 44,114 ndizo zinafaa kwa Kilimo, Hekta 57 zinafaa kwa ufugaji, Hekta 38,194 ni misitu ya asili na ya kupandwa na hekta 16,492 zinafaa kwa malisho ya mifugo ,hekta 45,143 ni eneo la maji ,milima na miamba.
Utawala
Kiutawala Wilaya imegawanyika katika Tarafa 5, Kata 27, Vijiji 68 na Vitongoji 296. Aidha Kata moja ya Kelamfua Mokala imekuwa Mamlaka ya Mji Mdogo wa Mkuu yenye jumla ya Mitaa 15. Wilaya ina Jimbo moja la Uchaguzi.
Hali ya Hewa
Wilaya ina majira ya Mvua za vuli yanayoanza mwezi Oktoba na kuishia mwezi Desemba na mvua za masika Machi hadi Mei na majira ya Kiangazi yanayoanza mwezi Juni na kuishia Oktoba. Wastani wa mvua kwa mwaka ni mm 1000 na wastani wa joto ni 220C.
Wilaya imegawanyika katika kanda 3 ambazo ni:-
Idadi ya Watu
Idadi ya watu kwa mujibu wa Sensa ya Kitaifa ya Watu na Makazi mwaka 2012 Wilaya ina watu 260,963, Wanaume 124,528 na Wanawake 136,435 na wastani wa watu 4 kwa kila Kaya. Aidha uchambuzi wa taarifa mbalimbali za Sensa ikiwa ni pamoja na ongezeko la watu kwa mwaka unafanyika na Ofisi ya Taifa ya Takwimu.
Shughuli za Kiuchumi
Asilimia 90 ya wakazi wa Wilaya ya Rombo wanajishughulisha na kilimo na mifugo, asilimia 7 ni wafanyabiashara/wajasiriamali na asilimia 3 ni watumishi katika sekta mbalimbali za umma na binafsi. Pato la mwananchi kwa Wilaya ya Rombo ni Tshs 850,000/=kwa mwaka kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012.
Rombo District Council,Mkuu Bomani Street
Sanduku la Posta: P.o Box 52,Mkuu,Rombo
Simu: 027-2757101
Simu ya Mkononi: 027-2757101
Barua Pepe: ded@rombodc.go.tz
Copyright@2019Rombodc.all rights reserved