Wilaya kupitia Idara ya Maji hushughulika na utekelezaji wa mipango ya muda mrefu na mfupi ya usambazaji wa maji katika maeneo ya mijini na vijijini ikishirikiana na kampuni inayosimamia huduma ya maji wilayani KILIWATER.
Huduma ya maji katika Wilaya ya Rombo inatolewa katika vijiji 68 kwa wakazi wapatao 260,963, wilaya ina vyanzo vya maji 30 kati ya hivyo vyanzo 29 ni vya maji ya mtiririko na vyanzo vitano (1) ni visima virefu.
Kiasi cha maji kinachozalishwa kwa siku ni mita za ujazo 27,000 kipindi cha masika na kwa kipindi cha kiangazi kiasi hicho hupungua na kufikia mita za ujazo 22,000, wakati mahitaji ya siku ni mita za ujazo 40,000. Mtandao wa mabomba unakadiriwa kufikia kilometa 1,300.
Idaya ya Maji inatekeleza Programu ya Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RWSSP)
Lengo la utekelezaji wa programu hii ni kuwapatia wananchi huduma ya maji katika umbali usiozidi mita 400, au kutumia muda usiozidi dakika 30 kwenda kuchota maji na kurudi nyumbani. Kwenye awamu ya kwanza ya Utekelezaji wa Programu ya Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (Rural Water Supply and Sanitation Programme-RWSSP) kwa Vijiji kumi kwa wilaya ya Rombo ulihusisha kijiji cha Ngoyoni, Ngareni, Shimbi Mashariki, Ushiri, Mahorosha, Msaranga, Kahe, Leto, Kiraeni na Urauri.
Teknolojia iliyopendekezwa na wananchi chini ya ushauri wa wataalam ni uchimbaji wa visima virefu (Boreholes) kwa vijiji tisa na maji ya mtirirko kwa kijiji kimoja tu cha ushiri.
Uchimbaji wa visima hivyo ulifanywa na mkandarasi Water Solution Drilling Co.ltd chini ya usimamizi wa Mtaalam Mshauri Norplan Tz Ltd.
Hali halisi ya utekelezaji wa Programu ya Maji na Usafi wa Mazingira vijijini
Uchimbaji wa visima virefu katika vijiji vya Kahe, Kiraeni, Mahorosha, Msaranga, Ngoyoni, Urauri, Shimbi-Mashariki, Leto na Ngareni ulikamilika, ambapo kati ya vijiji hivyo visima vilivyopata maji ya kutosha ni kijiji cha Kahe na Shimbi- Mashariki hivyo kuendelezwa kwa kujengewa miundombinu. Kwa vijiji vilivyochibwa visima virefu na kukosa maji( Dry borehole) ilitafutwa njia mbadala kwa kutoa maji kwenye bomba kubwa la maji toka vyanzo vya msitu wa Kinapa marangu.
Ujenzi wa miundombinu ya maji katika vijiji vya Mahorosha, Msaranga, Kiraeni na Ngoyoni umekamilika na wananchi wanapata huduma ya Maji.
Ujenzi wa miundombinu ya maji kwa vijiji vya Kahe na Ushiri imekamilika na huduma inaendelea kutolewa.
Miradi ya maji katika kijiji cha Shimbi – Masharaki, Ngareni na Leto wakandarasi walianza kazi mwezi Julai 2015. Katika vijiji vyote vitatu vyanzo vya maji ni visima virefu hivyo zitatumika pump (Pumped scheme).Miradi hii inatekelezwa kwa awamu.
Awamu ya Kwanza ilikuwa ujenzi wa:-
Awamu ya Pili ilikuwa ujenzi wa;
Kwasasa wakandarasi wote wameshajenga matenki ya kuhifadhia maji yenye lita 150,000 kwa kijiji cha Shimbi Mashariki na Leto na lita 75,000 na 25,000 kwa kijiji cha Ngareni.Jumla ya vituo vya kuchotea maji 56 vimejengwa Wakandarasi wanaendelea na kazi za umaliziaji wa miradi hiyo.
Mafanikio
Mikakati
Rombo District Council,Mkuu Bomani Street
Sanduku la Posta: P.o Box 52,Mkuu,Rombo
Simu: 027-2757101
Simu ya Mkononi: 027-2757101
Barua Pepe: ded@rombodc.go.tz
Copyright@2019Rombodc.all rights reserved