PROFILE YA IDARA YA UJENZI
1.0 Utangulizi:
Idara ya Ujenzi ni moja kati ya Idara kumi na nne za Halmashauri. Idara imegawanyika katika sehemu kuu mbili ambazo ni (i) Majengo na (ii) Umeme na Mitambo.
Idara ina watumishi wapatao kumi na sita (12) ambapo kati ya hao, Mkadiriaji majenzi (QS) 1, Mafundi Sanifu 2, Mafundi Sanifu wasaidizi 6, dereva 1, Walinzi 2.
Jukumu kuu la Idara ya Ujenzi ni Usimamizi na Ujenzi wa miundo mbinu katika Wilaya.
Sehemu hii inashughulika zaidi na usimamizi wa miradi mbalimbali ya majengo katika Wilaya ambapo miradi hii inatekelezwa na Idara mbalimbali za Halmashauri zikiwemo Utawala, Afya, Kilimo, Mifugo na Elimu.
Pia sehemu hii hutoa ushauri wa kitaalamu kwa jamii katika masuala yanayohusiana na ujenzi na ukarabati wa majengo. Aidha kwa kushirikiana na idara za Ardhi,maliasili na mazingira / Mipango miji na Afya Idara huratibu zoezi la utoaji wa vibali vya ujenzi wa majengo.
Sehemu hii inashughulika zaidi na ukaguzi na ukarabati wa mifumo ya umeme, magari na mitambo. Hata hivyo baada ya Serikali kubadili mfumo wa matengenezo ya magari na mitambo ambapo kwa sasa vinafanywa na wazabuni, sekta hii inashughulika na ukaguzi wa magari ya Halmashauri ili kubaini tatizo kabla ya kuyapeleka kwa wazabuni kwa matengenezo. Pia ukaguzi na usimamizi wa kazi za umeme katika miundo mbinu ya Halmashauri hufanywa na sehemu hii ya Idara.
Idara imefanikiwa kusimamia ujenzi na ukarabati mkubwa wa miundombinu ya sekta za Utawala, Afya, Elimu, Kilimo, Mifugo ambapo majengo ya Zahanati, Vituo vya Afya na nyumba za watumishi vimejengwa au kufanyiwa ukarabati.
Aidha shughuli za Kukagua na kusimamia shughuli zote za ujenzi wa majengo mbalimbali ndani ya Wilaya, Kutoa ushauri wa kitalaamu juu ya ujenzi bora na wa gharama nafuu na Kutoa elimu kuhusu kuzingatia sheria na kanuni za ujenzi vimefanikiwa kwa kiwango kikubwa.
Rombo District Council,Mkuu Bomani Street
Sanduku la Posta: P.o Box 52,Mkuu,Rombo
Simu: 027-2757101
Simu ya Mkononi: 027-2757101
Barua Pepe: ded@rombodc.go.tz
Copyright@2019Rombodc.all rights reserved