Mkuu wa wilaya ya Rombo Agness Hokororo awaasa wanafunzi wa kike wajionee huruma wasiharakie mambo yasiyowahusu kabla ya wakati, japokuwa kuna kesi chache za ubakaji lakini wengi wamekuwa wakienda maeneo yasiyowahusu na matokeo yake wanavuna kile walichokipanda.
Hayo aliyasema alipokuwa akihutubia katika maadhimisho ya juma la Elimu wilaya ya Rombo katika Viwanja vya shule ya sekondari Mkuu.
Aidha aliwaagiza walimu kuwajengea watoto wa jinsia zote uwezo kuanzia darasa la awali na kuendelea ili waweze kujua haki zao, maeneo wasiopaswa kushikwa, na vitendo wasivyopaswa kufanyiwa ili yakiwatokea waripoti kwa walimu wao.
Waratibu elimu kata na wakuu wa shule kuhakikisha mtoto anayethibitishwa na daktari kuwa na ujauzito asiondoke eneo la shule kabla ya kuripotiwa kituo cha polisi na awe amemtaja mhusika kabla hajarudi nyumbani ili kutovujisha siri na mtuhumiwa kutoroka.
“Wazazi,walezi, ,wadau wa elimu, wanafunzi wenyewe pamoja na serikali hatuzungumzi lugha moja katika kukemea na kupinga vitendo vya ukatili kwa watoto kitendo kinachosababisha kukatiza masomo kwa watoto wa kike na kushuka kwa kiwango cha taaluma”alisema Hokororo.
DC Hokororo ameliagiza jeshi la polisi kutosita kuwaweka ndani wazazi wa pande zote mbili iwapo wakishirikiana kuficha mhusika wa ujauzito mpaka pale atakapopatikana na kufikishwa mahakamani.
Afisa Elimu Sekondari(W) Petronila Wakurila amesema kuwa tatizo ya ulawiti ni kubwa kwa shule za msingi na tatizo la mimba za utotoni ni kubwa zaidi kwa shule za sekondari vitu vinavyoathiri saikolojia yao na kuhatarisha maendeleo ya taaluma pamoja na makuzi.
Aliongeza kuwa kwa kushirikiana na Idara ya Maendeleo ya jamii pamoja na Idara ya Afya wanaendelea kutoa elimu kwa jamii itakayosaidia kutokomeza matatizo ya ulawiti na mimba za utotoni.
Wilaya ya Rombo inakabiliwa na tatizo la wanafunzi kukatisha masomo kutokana na kupata ujauzito wakiwa shuleni ambapo kwa mwaka 2016 mimba 72 ziliripotiwa,mwaka 2017 mimba 64 ziliripotiwa na mwaka 2018 mimba 31 zimesharipotiwa japo jitihada kubwa ya kuondoa/ kupunguza mimba za utotoni zinafanywa bado hayajapatikana matunda ya kutosha.
Rombo District Council,Mkuu Bomani Street
Sanduku la Posta: P.o Box 52,Mkuu,Rombo
Simu: 027-2757101
Simu ya Mkononi: 027-2757101
Barua Pepe: ded@rombodc.go.tz
Copyright@2019Rombodc.all rights reserved