Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Dkt AveMaria Semakafu akizungumza katika mahafali ya chuo cha Maendeleo ya Wananchi Mamtukuna
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Dkt AveMaria Semakafu amesema sifa kuu ya kiongozi ni kuwa mbunifu, alipokuwa mgeni rasmi katika mahafali ya 30 chuo cha maendeleo ya wananchi Mamtukuna leo tarehe 12.10.2018.
Akizungumza katika hafla hiyo ameupongeza uongozi wa chuo pamoja na mwenyekiti wa bodi ya chuo ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji kwa kuwa wabunifu na kutumia wanafunzi wa chuo hicho kufanya kazi zinazoendelea katika wilaya kama vile ujenzi na ukarabati wa baadhi ya shule na zahanati, ikiwa kama sehemu ya mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi hao.
“Uongozi ni ubunifu sio umekuta kitu kinafanyika Januari hadi Januari ukasema hivi ndivyo inavyotakiwa kuwa , hapana, ukiwa kiongozi lazima uwe mbunifu”, amesema Semakafu
Semakafu amepongeza jitihada zilizofanyika za kuongeza fani zinazofundishwa katika chuo hicho kutoka fani mbili mpaka kufikia fani nane na mchakato wa chuo wa kuongeza fani nyingine mbili za uchomeleaji vyuma na fani ya kuongoza watalii (Tour Guide).
Wilaya ya Rombo ina njia ya Rongai kwenda Mlima Kilimanjaro hivyo uanzishwaji wa fani ya kuongoza watalii ipewe kipaumbele kwani inaweza kukipa chuo wateja wengi na kwa haraka, aliongeza Semakafu
Awali Kaimu Mkuu wa chuo hicho Ndg Rigamba Mwita akisoma taarifa ya chuo , ametaja mipango ya chuo hicho ni kuongeza fani ya uchomeleaji vyuma pamoja na fani ya kuongoza watalii kama watapata usaidizi pamoja na kuandaa mafunzo ya muda mfupi ya matumizi ya biogas kwa wananchi wa Rombo na viunga vyake ili kusambaza teknolojia rahisi inayoweza kuokoa misitu.
Aliongeza kuwa ,tayari chuo kinatumia nishati ya Biogas baada ya kufanikiwa katika zoezi la majaribio yaliyofanyika kwa ushirikiano wa Halmashauri ya Rombo na Manispaa ya Alyvnsbyn.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Dkt AveMaria Semakafu(wa pili kushoto wakifurahi kwa pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Rombo Magreth John( kulia) na Kaimu Mkuu wa chuo Rigamba Mwita (kushoto)
Rombo District Council,Mkuu Bomani Street
Sanduku la Posta: P.o Box 52,Mkuu,Rombo
Simu: 027-2757101
Simu ya Mkononi: 027-2757101
Barua Pepe: ded@rombodc.go.tz
Copyright@2019Rombodc.all rights reserved