Picha kwa hisani ya mtandao
Tamaduni mbalimbali zinazojumuisha imani,maadili,sanaa,sheria, desturi na mila, ambazo nyingine ni za kigeni na nyingine ni za kitanzania huchangia kwa kiasi kikubwa ukatili dhidi ya wanawake na watoto,hayo yalibainishwa katika ufunguzi wa Kamati ya kupiga vita ukatili dhidi ya wanawake na watoto katika wilaya ya Rombo na mtoa mada kutoka KWIECO(shirika lisilokuwa la kiserikali linalojihusisha na kuimarisha haki za binadamu na usawa wa kijinsia) Peter Mashingia.
Mashingia alisema kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto inaenda sambamba na kutokomeza mila na desturi kandamizi ,aliziorodhesha baadhi ya tamaduni hizo kuwa ni ukeketaji, mila na desturi zinazohamasishaji mimba za utotoni ,mila na desturi zinazohamasisha ndoa za lazima mtoto kuchaguliwa mme/mke akiwa shuleni, mume kumpiga mkewe kama ishara ya upendo.
‘ Tusijadili matokeo tuangalie nini hasa sababu ya haya matukio ya ukatili kutokea , wazazi wametawaliwa sana na shughuli za uchumi badala ya kusimamia makuzi ya watoto nyumbani na wengi wanaoleta haya matatizo ukichunguza anaishi na nani utakuta anaishi na babu au bibi,hivyo tunapozungumzia mazingira salama ni budi tujihoji wenyewe’. Mkuu wa Polisi Rombo Joseph Marwa alichangia.
Marwa aliongeza kuwa “Utamaduni wa kigeni unaathiri sana katika makuzi ya watoto kuna matukio yanatokea kwa sababu tumeruhusu sana utamaduni wa kigeni utawale maisha yetu, kuna mila ambazo wao wanaziona ni kandamizi lakini zilitusaidia na mimba za utotoni hazikuwepo”
Alimalizia kwa kusema kuwa, ulinzi wa jamii kwa mtoto kwa nyakati hizi ni mgumu tofauti na zamani ambapo mtoto alikuwa ni wa jamii nzima hata akikosea anaadhibiwa lakini kwa sasa ni ngumu kwa mtu kumchapa bakora mtoto wa jirani hata kama akimuona amekosea atajisemea shauri lake na wazazi wake.
Naye afisa maendeleo ya jamii wilaya Bi Restina Mwasha alisema timu zimeundwa kuanzia ngazi ya kijiji au mtaa kwa kujumuisha wataalamu kutoka sekta mbalimbali ili kufuatilia mnyororo mzima wa matukio ya ukatili yanayotokea katika maeneo yetu na kuyaripoti eneo husika.
Aliongeza kuwa huu ni mpango wa taifa uliopewa jina la MTAKUWWA (Mpango wa Taifa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto)ambao ni mpango utakaodumu kipindi cha miaka mitano kuanzia 2018 hadi 2022 lengo likiwa ni kutokomeza ukatili wa mama na mtoto kwa asilimia hamsini hivyo ili kuifikia asilimia hii ni budi ushiriki wetu uwe wa kina na matukio yaripotiwe.
Mbali na mikakati iliyowekwa na MTAKUWWA kamati ya ulinzi wa wanawake na watoto imeundwa kwa kufuata mwongozo ili kuboresha utoaji wa huduma kwa makundi yaliyo katika mazingira hatarishi, kwa kutoa elimu na kuhamasisha jamii kuhusu kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto, ikiwa ni pamoja na kutoa msaada wa kisheria kwa waathirika wa ukatili na kuimarisha mahusiano katika jamii.
Rombo District Council,Mkuu Bomani Street
Sanduku la Posta: P.o Box 52,Mkuu,Rombo
Simu: 027-2757101
Simu ya Mkononi: 027-2757101
Barua Pepe: ded@rombodc.go.tz
Copyright@2019Rombodc.all rights reserved