Katika kila kikao cha robo ya nne cha baraza la madiwani, ambacho ndicho kikao cha mwisho kwa mwaka wa fedha kuna utaratibu wa kuchagua upya wenyeviti na wajumbe wa kamati za kudumu za halmashauri pamoja na uchaguzi wa makamu mwenyekiti.
Aidha uchaguzi wa nafasi ya makamu mwenyekiti umeahirishwa kufanyika baada ya sintofahamu kuibuka katika kikao hicho ambapo wagombea wawili , mmoja kutoka chama cha CHADEMA Mhe. Nicholaus Kimario ambaye ameshikilia nafasi hiyo kwa vipindi vinne mfululizo na mgombea mwenza kutoka CCM Abdallah Mbago kwa kila mgombea kushindwa kufikisha asilimia hamsini ya kura zote.
Idadi ya wapiga kura walikuwa ni 36, ambapo uchaguzi ulipofanyika mhe. Kimario alipata kura 14, mhe. Mbago kura 4, kura 16 ziliharibika na kura 2 zilikosewa majina. Baada ya majadiliano muafaka ulifikiwa wa uchaguzi kurudiwa ambapo Mhe. Kimario alipata kura 17,Mhe. Mbago kura 2, kura 17 ziliharibika.
Katika uchaguzi huo ambao mshindi hakupatikana kutokana na sheria ndogo za halmashauri zinazosema mshindi anatakiwa awe amepata kura zaidi ya asilimia hamsini ,jambo lililosababisha kila chama kurudi kukaa upya kuchagua mgombea mwingine katika nafasi hiyo baada ya kuonekana kuwa wagombea walioletwa mbele ya baraza hawakupitishwa.
Sambamba na hilo baraza liliamua kuwa mara baada ya vyama kuteua upya wagombea wa nafasi hiyo, litaitishwa baraza maalumu kwa ajili ya kurudia uchaguzi huo.
Rombo District Council,Mkuu Bomani Street
Sanduku la Posta: P.o Box 52,Mkuu,Rombo
Simu: 027-2757101
Simu ya Mkononi: 027-2757101
Barua Pepe: ded@rombodc.go.tz
Copyright@2019Rombodc.all rights reserved