Kamishna msaidizi mwandamizi wa Jeshi la Polisi (SACP) SIMON MAIGWA ambaye ndiye Kamanda wa polisi Mkoa wa kilimanjaro Aprili 22, 2024 amefanya ziara katika Wilaya ya Rombo kwa mujibu wa sheria inayomtaka kufanya kaguzi za vituo vya polisi ili kujionea hali halisi ya ulinzi na usalama.
Hata hivyo kabla ya kuanza ziara yake kamanda SACP Maigwa alipokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Rombo Mhe. Raymond Mwangwala ambaye ndie mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama katika Wilaya
.
Mapokezi hayo yaliambayana na kikao kifupi kilichofanyika katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya kilicholenga kutoa taarifa na taswira kamili ya hali ya ulinzi na usalama katika wilaya ya Rombo.
Rombo District Council,Mkuu Bomani Street
Sanduku la Posta: P.o Box 52,Mkuu,Rombo
Simu: 027-2757101
Simu ya Mkononi: 027-2757101
Barua Pepe: ded@rombodc.go.tz
Copyright@2019Rombodc.all rights reserved