• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Halmashauri ya Wilaya ya Rombo
Halmashauri ya Wilaya ya Rombo

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali Za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Rombo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Ujenzi
      • Maji
      • Mipango na Takwimu
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Ardhi na Maliasili
      • Utumishi na Utawala
      • Afya
    • Kitengo
      • TEHAMA
      • Manunuzi na Ugavi
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Nyuki
      • Uchaguzi
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • maji
    • Elimu
    • Watumishi
    • Kilimo
    • Afya
    • Mifugo
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Mipya
  • Machapisho
    • Fomu
    • Sheria Ndogo
    • Ripoti
    • Taratibu
    • Taarifa za Fedha
      • Taarifa ya makisio ya Mapato
      • Taarifa ya Mapato Halisi
      • Taarifa ya Matumizi
      • MTEF
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Hotuba

Mkuu wa Wilaya ya Rombo Mhe. Raymond Steven Mwangwala tarehe April 22, 2024 amefanya mkutano wa hadhara wenye lengo la kusikiliza na kutatua kero za wananchi wa Tarafa ya Mengwe.

Posted on: April 22nd, 2024


Mkuu wa Wilaya ya Rombo Mhe. Raymond Steven  Mwangwala  tarehe   April 22, 2024 amefanya mkutano wa hadhara wenye lengo la kusikiliza na kutatua kero za wananchi wa Tarafa ya Mengwe.



Katika mkutano huo uliofanyika holili katika viwanja vya ofisi za mtendaji wa kata Mhe. Mwangwala aliambatana na kamati ya ulinzi na usalama, Wataalamu kutoka Halmashauri ya Wilaya  ya Rombo na wengine kutoka Taasisi zinazowahudumia wananchi kwa ukaribu ikiwemo Wakala wa Barabara za Vijijini na Mji (TARURA) , Wataalamu kutoka Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira (rombowasa) pamoja na wataalamu kutoka Shirika la Umeme Tanzania ( TANESCO). 


Katika kusikiliza kero za wananchi wa Tarafa Ya Mengwe kata ya holili ,  Mkuu wa wilaya alipokea changamoto mbalimbali zikiwemo zinazohusu  Elimu, Miundombinu ya barabara, Maji, Umeme, Afya, migogoro mbalimbali ya Ardhi na changamoto za Kisheria zinazowakabili wananchi hao.


 Mkuu wa Wilaya akishirikiana na wataalamu aliongozana nao walifanikiwa kutolea majibu kwa baadhi ya changamoto huku nyingine zikipaa utatuzi wa  papo kwa papo na nyingine zilipokelewa kwa maelekezo ya kupatiwa mwarobaini wake.


Hatahivyo, Dc Mwangwala amewataka viongozi wa TARURA  kurekebisha miundombinu ya barabara hasa maeneo yenye uhitaji zaidi kutokana na uharibifu ulosababishwa na mvua zilizonyesha.


Sambamba na hilo Dc Mwangwala  amesema suala la Usalama katika Wilaya sio jukumu la polisi peke yake bali ni jukumu  la kila mwananchi, hivyo amewataka wananchi kuwa mstari wa mbele katika kutoa ushirikiano endapo uhalifu utatokea ili kusaidia kutunza amani na usalama hasa maeneo hayo ambayo yapo mpakani na nchi jirani ya Kenya.


Naye Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Rombo  amemuhakikishia Mkuu wa Wilaya kutatua kero  kwa wakati

 “Tutahakikisha kero hizi tunazitatua kwa wakati bila kuathiri maeneo mengine kwani Wataalamu wetu tumewaelekeza kufuatilia maeneo yote yenye kero na kushughulikia kwa wakati hususani eneo la elimu, Ustawi wa Jamii, Maendeleo ya Jamii pamoja na eneo la sheria hivyo nipende kutoa shukrani zangu kwa Mkuu wa Wilaya  kwa ziara hii ya kutatua kero na nikuhakikishie tumejipanga kuondoa kero za wananchi kwa ajili ya kukuza uchumi wao.”


Matangazo

  • MATOKEO YA USAHILI WA WALIOOMBA KAZI YA KUKUSANYA MAPATO NA KAZI YA USAFI August 27, 2024
  • TANGAZO LA UUZAJI WA VIWANJA VYA HALMASHAURI YA WILAYA YA ROMBO June 14, 2024
  • TANGAZO LA MNADA WA HADHARA August 26, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI YA AJIRA YA MKATABA July 16, 2024
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • KARIBU KWENYE BARAZA LA MADIWANI.

    May 07, 2025
  • KARIBU KWENYE BARAZA LA MADIWANI.

    May 07, 2025
  • ZAID YA SHILINGI MILIONI MIA SITA AROBAINI NA MOJA YA KABIDHIWA KWA VIKUNDI 52

    April 17, 2025
  • ZAID YA SHILINGI MILIONI MIA SITA AROBAINI NA MOJA YA KABIDHIWA KWA VIKUNDI 52

    April 17, 2025
  • Ona Zote

Video

Maafisa Elimu Kata wakizifanyia Majaribio Pikipiki
Video Zaidi

Viunganishi Vya Haraka

  • Muundo wa Halmashauri
  • Wasiliana Nasi Kwa
  • Miladi iliyokamilika

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • MFUMO WA TAUSI
  • Ffars
  • Tamisemi
  • Idara ya Takwimu (NBS)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Rombo District Council,Mkuu Bomani Street

    Sanduku la Posta: P.o Box 52,Mkuu,Rombo

    Simu: 027-2757101

    Simu ya Mkononi: 027-2757101

    Barua Pepe: ded@rombodc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright@2019Rombodc.all rights reserved