Baraza la madiwani wa halmashauri ya Wilaya ya Rombo wafanya kikao cha kufunga mwaka wa fedha 2022/23, nae Mkuu wa mkuu wa wilaya ya Rombo mhe. Kanali Hamis Maiga, mkuu Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Nurdin Babu Pamoja na akatibu tawala mkoa wa Kilimanjaro mhe. Tixon Nzunda wahudhuria kikao hicho kilicholenga kujibu hoja za mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (CAG).
Baraza hilo la waheshimiwa madiwani lilipitia hoja 10 silizosalia kujibiwa kati ya hoja 31 zilizohitaji majibu na baada ya majadiliano na mapitio ya hoja hizo kwa kina waliridhia mpaka ifikapo mwezi wa saba hoja hizo ziwe zimekamilishwa kujibiwa, lakini pia kuwepo na vielelezo na kufunga hoja hizo.
Hata hivyo, Kabla ya kikao hicho kuhairihswa mwenyekiti wa kikao hicho Pamoja mkurugenzi alimkaribisha kuu wa wilaya ambaye alimkaribisha katibu tawala azungumze jambo na baraza hilo la madiwani. “Kwanza niwapongeze kwa kuwa halmashauri iliyokusanya mapato kwa Zaidi ya asilimia 100 lakini nisisitize ufungwaji wa vifaa vya kieletroniki kwenye vyanzo vyote vya mapato ambapo itasaidia kupunguza upotevu wa mapato” alishauri katibu tawala mhe. Tixon Nzunda.
Vile vile Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Babu alishauri baraza hilo la madiwani kuhakikisha wanasimamai utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika kila kata. Pia akiomba kila diwani kwa nafasi yake kuhakikisha wanapambana kutokomeza mmomonyoko wa maadili ambao kwa sasa imekuwa changamoto kubwa nchini na duniani kiujumla.
Rombo District Council,Mkuu Bomani Street
Sanduku la Posta: P.o Box 52,Mkuu,Rombo
Simu: 027-2757101
Simu ya Mkononi: 027-2757101
Barua Pepe: ded@rombodc.go.tz
Copyright@2019Rombodc.all rights reserved