Wanawake wa wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro wameanzisha mfuko wa jukwaa la kiuchumi kwa wanawake wenye lengo la kuwasaidia kisheria na kiuchumi wanawake na watoto wanaobakwa, kulawitiwa na kufanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia ili wapate haki zaona wahusika wachukuliwe hatua za kisheria baada ya kugunduliwa kwa waathirika wengi hawana uwezo. Jukwaa na Mfuko huo umefumguliwa rasmi na mgeni rasmi mhe. Shally J Raymond mbunge wa viti maluum.
Aidha, katika maadhimisho hayo ya wanawake duniani wilayani Rombo, mwenyekiti wa jukwaa hilo Bi. Evomia Masika ametolea ufafanuzi wa kina kuhusu mfuko huo,yakua utahudumia kata zote 28 za Rombo ili kutokomeza vitendo hivyo ambavyo vimekithiri katika jamii.
Rombo District Council,Mkuu Bomani Street
Sanduku la Posta: P.o Box 52,Mkuu,Rombo
Simu: 027-2757101
Simu ya Mkononi: 027-2757101
Barua Pepe: ded@rombodc.go.tz
Copyright@2019Rombodc.all rights reserved