Idara ya elimu, wadau wa elimu pamoja na viongozi mbalimbali wa halmashauri ya wilaya ya Rombo, wamefanikiwa kufanya kikao cha tathmini ya mwenendo wa matokeo ya kidato cha pili na kidato nne. Kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa shule ya saint joseph iliyopo mkuu, Rombo kililenga kufikia ufaulu wa asilimia 100 kwa wanafunzi wa elimu ya sekondari kwakuwa ndipo maarifa ya msingi katika uhai na ufanisi wa maisha ya mwanadamu yalipo.
Moja ya agenda katika kikao hiko kilichohudhuriwa na wadau wa elimu mbalimbali ikiwemo waalimu, waalimu wakuu, wakuu wabodi ya shule, maafisa elimu kata na waheshimiwa madiwani, ilikuwa ni kupata taarifa ya elimu na umuhimu wa wadau wa elimu katika kuhakikisha wanafunzi wanapata kile wanachostahili kupata shuleni.
Hata hivyo kikao hiko kilifanikiwa kuweka makubaliano ya kimkakati ya kuongeza ufaulu kwa mwaka 2023 endapo yatafanyiwa utekelezaji unaoendana na kauli mbiu isemayo “MBINU SHIRIKISHI UWAJIBIKAJI UTAWEZESHA YALIYOSHINDIKANA YAWEZEKANE”.Yafuatayo ni makubaliaono ya kimakakati yaliyopitishwa na wadau wa elimu ambayo ni pamoja na
Aidha, afisa taaluma sekondari wailaya ambaye ndiye aliyekuwa mwenyekiti wa kikao hicho , aliendesha majadiliano na maazimio na wadau hao wa elimu na kusema kuwa, wilaya imejipanga kutoa motisha chanya ya Tsh 5,000/= kwa kila “A” halali, na hadi sasa Tsh 5,000,0000/= zimeshaanza kukusaanywa kwaajili ya zawadi kwa wadau wote wa elimu watakao faulisha kwa ufaulu wa asilimia 100. Lengo la utoaji wa zawadi likiwa ni kuongeza na kuchochea ufaulu kwani tathimini ya mwenendo na hali ya matokeo kiujumla hairidhishi hivyoo amewaasa wadau wote wa elimu kuchukua kwa uzito utekelezaji wa majukumu yao kama wadau wa elimu.
Katika kikao hicho mlw. Charles Daudi Mganga (Kaimu Mkurugenzi) alifanikiwa kutoa nasaa zake na kuwaasa sana waalimu kujitoa kikamilifu katka kutekeleza majukumu yao kwani waalimu ndio wenye mchango mkubwa kuahakikisha ufaulu wa asilimia 100 kama yalivyo malenge.
Hata hivyo naye aliyekuwa mgeni rasmi ambae ni Katibu wa mbunge aliongeza kwa kuwatia moyo wadau wa elimu na kuahidi kuchukuwa changamoto zilizotajwa na wadau wa elimu na kuwahakikishia atazipeleka mahala husika zipatiwe mwarobaini.
Hali kadhalika Katika kikao hicho, ,halmashauri ya wilaya ya Rombo kupitia idira ya elimu, ilifanikiwa kutoa vyeti na zawadi mbalimbali, ikiwemo mitungi ya gesi, sukari na mchele kwa shule zilizofanyanya vizuri, pia kwa shule zilizoonyesha jitihada na mjongeo chanya katika matokeo ya kidato cha pili na cha nne ya mwaka 2022.
Kwa taarifa zaidi kuhusu tathimini hiyo unaweza ukaipata hapa
Rombo District Council,Mkuu Bomani Street
Sanduku la Posta: P.o Box 52,Mkuu,Rombo
Simu: 027-2757101
Simu ya Mkononi: 027-2757101
Barua Pepe: ded@rombodc.go.tz
Copyright@2019Rombodc.all rights reserved