Mkuu wa wilaya ya rombo awataka wadau wa elimu wilaya ya Rombo kuhakikisha wanawasaidia watoto wenye ulemavu wa akili ,wasioona, ulemavu mchanganyiko pamoja na viziwi kupata haki zao za msingi ili nao waandikishwe kwenye vituo vya elimu.
Hayo aliyasema DC Agness Hokororo alipokuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya juma la elimu wilayani Rombo katika shule ya Mkuu sekondari.
Aliongeza kuwa wazazi wanawaficha watoto wenye ulemavu majumbani kitu ambacho sio sahihi kwani kwa kuwasikiliza walimu wao inaonesha kuwa watoto hawa wanafundishika na wana uwezo wa kujifunza stadi mbalimbali.
Naye Afisa elimu sekondari (W) Bi. Petronila Wakurila alisema kuwa watoto wenye ulemavu wanafatiliwa kwa karibu sana na idara ya Elimu. Na mpaka sasa kuna watoto 32 waliosajiliwa katika shule ya msingi Klenki, 86 wanasoma katika shule na vitengo maalumu na 164 wanasoma katika shule za kawaida.
Wakurila alielezea changamoto ya ukosefu wa mabweni kwa watoto wenye ulemavu ila DC Hokororo alimtoa hofu kwa kumhakikishia changamoto hiyo inashughulikiwa ili kujengwa bweni angalau katika kituo kimoja ili watoto wenye ulemavu waende kwenye kituo hicho.
Aidha lengo la serikali ya awamu ya tano katika sekta ya elimu ni kuzalisha maarifa na stadi mbalimbali ambazo zitachochea mapinduzi ya kiuchumi na kuiwezesha Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025, kupitia sekta ya viwanda, alisema Hokororo
“Elimu ni mchakato unaomuwezesha mwanadamu kupata taarifa ,ujuzi, maadili na mabadiliko ya kudumu kuhusu tabia na mwenendo ili aweze kuyamudu na kuyatawala mazingira yake,hivyo Elimu ni sekta muhimu kimkakati katika kuandaaa rasilimali watu walioelimika ambao watawezesha malengo ya kufikia uchumi wa viwanda” ,alimalizia Hokororo.
Hali ya ufaulu katika wilaya ya Rombo ni ya Wastani, kwani inajitahidi kuongeza ufaulu katika mjongeo mdogo sana ukilinganisha na wilaya nyingine kwa mfano ufaulu wa kidato cha pili 2016 ni 91.2% na 2017 ni 92.7%, wakati kidato cha nne 2016 72.8%ni na 2017 ni 81.8%.
Rombo District Council,Mkuu Bomani Street
Sanduku la Posta: P.o Box 52,Mkuu,Rombo
Simu: 027-2757101
Simu ya Mkononi: 027-2757101
Barua Pepe: ded@rombodc.go.tz
Copyright@2019Rombodc.all rights reserved