MKUU wa wilaya ya Rombo Bi Agness Hokororo amefanya ziara pamoja na kamati ya ulinzi na usalama na timu ya wataalamu wa halmashauri, kupitia na kukagua miradi ya maendeleo ambapo ameridhishwa na uwiano uliopo kati ya miradi na thamani ya fedha zilizotumika.
Pamoja na kumpongeza DED na timu ya wataalamu, Bi Hokororo amewaagiza kufuatilia kwa karibu miradi inayoendelea kutekelezwa kwa kwenda vijijini kusimamia wakandarasi na si kuwaachia watendaji waliopo kwenye ofisi za vijiji.
Baada ya ziara ndefu ya kutembelea miradi ya afya, shule na ofisi za vijiji BI Hokororo alihitimisha kwa kutoa angalizo kuwa 'ni lazima fedha ya serikali ya walipa kodi, wakulima na wafanyakazi katika Jamhuri ya Muungano ya Tanzania ionekane,mara nyingi wataalamu wamekuwa si waaminifu na hili hatukubaliani nalo'.
Rombo District Council,Mkuu Bomani Street
Sanduku la Posta: P.o Box 52,Mkuu,Rombo
Simu: 027-2757101
Simu ya Mkononi: 027-2757101
Barua Pepe: ded@rombodc.go.tz
Copyright@2019Rombodc.all rights reserved