Mkuu wa Wilaya ya Rombo Mh.Raymond Mwangwala @mwl_mwangwala amemkabidhi Mtumishi Sixmund Joseph Ngoo Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Mahida Cheti Cha kuthamini (Certificate of Appreciation) kwa mchango wake Bora katika kuwahudumia Wananchi kwa kutoa Huduma Bora za Afya kwa Wananchi wa Mahida.
Aidha Mh.Mwangwala ametumia fursa hiyo kuwaasa Watoa Huduma za Afya kutoa Huduma bora za Afya kwa weledi pamoja na kuwa na kauli nzuri kwa Wagonjwa pale wanapowahudumia.
Rombo District Council,Mkuu Bomani Street
Sanduku la Posta: P.o Box 52,Mkuu,Rombo
Simu: 027-2757101
Simu ya Mkononi: 027-2757101
Barua Pepe: ded@rombodc.go.tz
Copyright@2019Rombodc.all rights reserved