Kilimo
Wilaya ya Rombo ina jumla ya Ha 44,114 zinazofaa kwa kilimo. Kati ya hizo Hekta 18,168 zinalimwa mazao ya kudumu (Migomba, kahawa) Eneo lililobakia linatumika kwa kilimo cha mazao ya msimu kama inavyoonekana kwenye jedwali hapa chini:
Mazao yanayolimwa
Aina ya Zao Eneo linalolimwa
1 Kahawa na Migomba 15,950
2 Migomba pekee (pure stand) 2000
3 Kahawa peke (pure stand) 68
4 Mahindi 12,000
5 Maharage 6000
6 Kunde 128
7 Mbaazi 400
8 Alizeti 900
9 Karanga 450
10 Magimbi 400
11 Ulezi 1760
12 Mtama 200
13 Mhogo 670
14 Viazi Mviringo 2650
15 Viazi vitamu 200
16 Choroko 100
17 Mboga 88
18 Matunda 150
Jumla 44,114
Hali ya hewa
Wilaya ya Rombo ina Misimu miwili ya mvua ambayo ni Vuli na Masika. Msimu wa Vuli huanza mwezi Oktoba hadi Desemba. Msimu huu ndio unaotegemewa zaidi na wakulima.
Msimu wa Masika huanza mwezi Machi hadi Mei kila mwaka. Wilaya ina Kanda tatu (3) za kilimo ambazo ni Ukanda wa Juu, Ukanda wa Kati na Ukanda wa chini.
Ukanda wa juu upo kati ya mita 1,200 hadi mita 1,800 juu ya usawa wa bahari. Aina ya udongo inayopatikana katika Ukanda huu ni 'Volcanic soil' na Mazao yanayolimwa katika Ukanda huu ni kahawa, migomba na mahindi ya muda mrefu viazi mviringo, pamoja na mboga na matunda(parachichi). Pia sehemu kubwa ya Ukanda huu ni eneo la Msitu. Hali ya hewa katika Ukanda huu; mvua ni kati ya 1000mm hadi 1500mm na nyuzi joto 150C hadi 200 C. Ukanda huu una msongamano mkubwa wa watu (kaya 480-500 kwa kilomita moja ya eneo (/km2).
Ukanda wa kati upo kati ya mita 900m- 1,200 juu ya usawa wa bahari. Udongo uliopo katika ukanda huu ni mchanyiko wa mfinyanzi na mboji. Hali ya joto katika ukanda huu ni kati ya nyuzi joto 200-300 C, Mazao yanayolimwa katika Ukanda huu ni pamoja na kahawa, migomba, mahindi ya muda mfupi, mazao ya jamii zote za kunde, matunda hasa maembe, alizeti, Mhogo, Karanga na mtama.
Ukanda wa chini upo chini ya mita 900 juu ya usawa wa bahari.Hali ya hewa katika Ukanda huu ni joto(250C -300C) pamoja na ukame wa mara kwa mara. Aina ya udongo katika ukanda huu ni udongo mchanganyiko (variable textures from sandy clay to loams).
Hali ya kilimo/Agriculture potentials
Wakulima wengi bado wanatumia jembe la mkono kwenye kilimo chao kutokana na hali halisi ya mashamba yao kuwa madogo(kati ya 1/2 Ekari hadi Ekari1. Matumizi ya matrekta na wanyama kazi yapo kwa kiwango kidogo. Wakulima wameshauriwa kutumia zaidi matrekta madogo (power tillers) ambapo jumla ya matrekta madogo 14 yapo na yanafanya kazi katika maeneo mbalimbali ya wilaya. Trekta hizo zinamilikiwa na vikundi vilivyowezeshwa na Serikali, Taasisi na watu binafsi. Kilimo chetu kinahitaji matumizi makubwa ya mbolea hasa samadi kutokana na mashamba kulimwa mfululizo bila kupumzishwa.Hii imetokana na kuwepo kwa misimu miwili ya mvua na udogo wa mashamba ambao unawalazimisha wakulima kulima kwa misimu yote miwili bila kupumzisha mashamba yao.
Kahawa bado ndio zao kuu la biashara la wilaya ya Rombo ambapo kati ya tani 2,000 hadi 3000 huvunwa kwa mwaka. Ndizi pamoja na kuwa zao la chakula lakini linachangia kwa kiasi kikubwa kipato cha wakulima. Uzalishaji wa ndizi uko juu kutokana na mbegu bora za migomba aina za williams, chinese cavendish na lacatan. Wastani wa tani 191,400 huzalishwa kila mwaka ambapo asilimia 70% huuzwa katika masoko mbalimbali ya ndani na nje ya wilaya na asilimia 30% hutumika kwa matumizi ya nyumbani (chakula).
Rombo District Council,Mkuu Bomani Street
Sanduku la Posta: P.o Box 52,Mkuu,Rombo
Simu: 027-2757101
Simu ya Mkononi: 027-2757101
Barua Pepe: ded@rombodc.go.tz
Copyright@2019Rombodc.all rights reserved