• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Halmashauri ya Wilaya ya Rombo
Halmashauri ya Wilaya ya Rombo

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali Za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Rombo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Ujenzi
      • Maji
      • Mipango na Takwimu
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Ardhi na Maliasili
      • Utumishi na Utawala
      • Afya
    • Kitengo
      • TEHAMA
      • Manunuzi na Ugavi
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Nyuki
      • Uchaguzi
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • maji
    • Elimu
    • Watumishi
    • Kilimo
    • Afya
    • Mifugo
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Mipya
  • Machapisho
    • Fomu
    • Sheria Ndogo
    • Ripoti
    • Taratibu
    • Taarifa za Fedha
      • Taarifa ya makisio ya Mapato
      • Taarifa ya Mapato Halisi
      • Taarifa ya Matumizi
      • MTEF
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Hotuba

Elimu bora nyenzo kuu kwa maendeleo ya Taifa

Posted on: August 1st, 2018

Mkuu wa wilaya ya rombo awataka wadau wa elimu  wilaya ya Rombo kuhakikisha wanawasaidia watoto wenye ulemavu wa akili ,wasioona, ulemavu mchanganyiko pamoja na viziwi kupata haki zao za msingi  ili nao waandikishwe kwenye vituo vya elimu.

Hayo aliyasema DC Agness Hokororo alipokuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya juma la elimu wilayani Rombo katika shule ya Mkuu sekondari.

Aliongeza kuwa wazazi wanawaficha watoto wenye ulemavu majumbani kitu ambacho sio sahihi kwani kwa kuwasikiliza walimu wao inaonesha kuwa watoto hawa wanafundishika na wana uwezo wa kujifunza stadi mbalimbali.

Naye Afisa elimu sekondari (W) Bi. Petronila Wakurila alisema kuwa watoto wenye ulemavu wanafatiliwa kwa karibu sana na idara ya Elimu. Na mpaka sasa kuna watoto 32 waliosajiliwa katika shule ya msingi Klenki, 86 wanasoma katika shule na vitengo maalumu na 164 wanasoma katika shule za kawaida.

Wakurila alielezea changamoto ya ukosefu wa mabweni  kwa watoto wenye ulemavu ila DC Hokororo alimtoa hofu  kwa kumhakikishia changamoto hiyo inashughulikiwa ili kujengwa bweni angalau katika kituo kimoja ili watoto wenye ulemavu waende kwenye kituo hicho.

Aidha lengo la serikali ya awamu ya tano katika sekta ya elimu ni kuzalisha maarifa na stadi mbalimbali ambazo zitachochea mapinduzi ya kiuchumi na kuiwezesha Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025, kupitia sekta ya viwanda, alisema Hokororo

“Elimu ni mchakato unaomuwezesha mwanadamu kupata taarifa ,ujuzi, maadili na mabadiliko ya kudumu kuhusu tabia na mwenendo ili aweze kuyamudu na kuyatawala mazingira yake,hivyo Elimu  ni sekta muhimu kimkakati katika kuandaaa rasilimali watu walioelimika ambao watawezesha malengo ya kufikia uchumi wa viwanda” ,alimalizia Hokororo.

Hali ya ufaulu katika wilaya ya Rombo ni ya Wastani, kwani inajitahidi kuongeza ufaulu katika mjongeo mdogo sana ukilinganisha na wilaya nyingine kwa mfano ufaulu wa kidato cha pili 2016 ni 91.2% na 2017 ni 92.7%, wakati kidato cha nne 2016 72.8%ni na 2017 ni 81.8%.



Matangazo

  • MATOKEO YA USAHILI WA WALIOOMBA KAZI YA KUKUSANYA MAPATO NA KAZI YA USAFI August 27, 2024
  • TANGAZO LA UUZAJI WA VIWANJA VYA HALMASHAURI YA WILAYA YA ROMBO June 14, 2024
  • TANGAZO LA MNADA WA HADHARA August 26, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI YA AJIRA YA MKATABA July 16, 2024
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • KARIBU KWENYE BARAZA LA MADIWANI.

    May 07, 2025
  • KARIBU KWENYE BARAZA LA MADIWANI.

    May 07, 2025
  • ZAID YA SHILINGI MILIONI MIA SITA AROBAINI NA MOJA YA KABIDHIWA KWA VIKUNDI 52

    April 17, 2025
  • ZAID YA SHILINGI MILIONI MIA SITA AROBAINI NA MOJA YA KABIDHIWA KWA VIKUNDI 52

    April 17, 2025
  • Ona Zote

Video

Maafisa Elimu Kata wakizifanyia Majaribio Pikipiki
Video Zaidi

Viunganishi Vya Haraka

  • Muundo wa Halmashauri
  • Wasiliana Nasi Kwa
  • Miladi iliyokamilika

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • MFUMO WA TAUSI
  • Ffars
  • Tamisemi
  • Idara ya Takwimu (NBS)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Rombo District Council,Mkuu Bomani Street

    Sanduku la Posta: P.o Box 52,Mkuu,Rombo

    Simu: 027-2757101

    Simu ya Mkononi: 027-2757101

    Barua Pepe: ded@rombodc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright@2019Rombodc.all rights reserved