• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Halmashauri ya Wilaya ya Rombo
Halmashauri ya Wilaya ya Rombo

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali Za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Rombo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Ujenzi
      • Maji
      • Mipango na Takwimu
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Ardhi na Maliasili
      • Utumishi na Utawala
      • Afya
    • Kitengo
      • TEHAMA
      • Manunuzi na Ugavi
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Nyuki
      • Uchaguzi
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • maji
    • Elimu
    • Watumishi
    • Kilimo
    • Afya
    • Mifugo
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Mipya
  • Machapisho
    • Fomu
    • Sheria Ndogo
    • Ripoti
    • Taratibu
    • Taarifa za Fedha
      • Taarifa ya makisio ya Mapato
      • Taarifa ya Mapato Halisi
      • Taarifa ya Matumizi
      • MTEF
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Hotuba

Vivutio vya Utalii

FURSA ZA UTALII

Katika Wilaya kuna maeneo mbalimbali ambayo ni vivutio vya utalii. Maeneo hayo ni pamoja na Ziwa Chala, Vilele vya Mlima Kilimanjaro (Mawenzi na Kibo), Kaburi la Mangi Horombo na Mahandaki yaliyotumika kama maeneo ya maficho wakati wa Vita.

  Ziwa Chala

Ziwa hili lipo mpakani mwa Nchi ya Kenya na Tanzania takribani kilomita 45 kutoka barabara ya Moshi- Taveta; kwa kuingilia eneo la Holili

Ziwa Chala lilitokana na mlipuko wa volkano ambalo limedidimia kwa muonekano. Ziwa hili linasemekana kuwa na muunganiko wa kijiolojia na mlima Kilimanjaro. Ziwa lina takribani kina cha mita 3,000 ambapo hadi sasa hakuna utafiti wa kisanyansi unaothibitisha urefu wa kina cha ziwa hili ambalo lina mvuto wa kipekee kwani hakuna mto unaoingiza, wala kutoa maji.  Ni ziwa lenye maji baridi na samaki wa maji baridi.

 Eneo la Ziwa Chala, kuna hekta zipatazo 23(ishirini na tatu) kwa upande wa Tanzania ambazo ni mashamba yanayomilikiwa na watu binafsi  eneo hili linaweza kutumika katika ujenzi wa mahoteli na “campsite”.

Aidha tunahita wananchi wa Ndani na Nje ya Nchi ili waje kufanya utalii kwa kujionea maajabu ya umbile la ziwa hilo. Huduma za Hoteli zinapatikana kwa kuwa limepakana na hoteli ya kitalii inayojulikana kwa jina la lake Chala safari Lodge.

Vilele vya Mlima Kilimanjaro

Vilele vya mlima huu vinapatikana Wilaya ya Rombo. Njia inayotumika kupandia mlima Kilimanjaro ambayo ipo Rombo inajulikana kwa jina la Nalemuru route. Ili kufika njia hii ni km. 95 toka Moshi Mjini. Njia hii inapitika kwa urahisi na ina vivutio vya wanyama mfano Mbega, Tembo, Nyani, Kima, Tumbili, Ng’edere, Ngiri, Simba wachache, Mbwa mwitu, Mbweha na Wanyama wengine.

Kuna vituo vitatu kwa kupitia njia hii:-

1.    Simba Camp     2ndcave       3rdcave       Kibo        halfSummit

2.    Samba Camp         2nd  cave          Kikelelwa     cave    Mawenzi      half     Kibo        half  Summit

3.    Samba cave       2nd cave        3rd cave         School       half         Barafu      Summit

•    Ni njia rahisi kuliko zote za kupandia Mlima Kilimanjaro, haina mwinuko sana ni njia ambayo ukiwa unapanda unaweza kuona Mbuga ya wanyama Amboseli iliyopo Kenya na Wilaya ya Kajiado kwa urahisi. Wakati unapanda unatumia siku tano (5) kupanda mlima huu. Kwa njia ya Marangu unaweza kutumia siku (6 – 7)

•    Kwa njia hii utapanda na kushukia Marangu, vile vile kwa kutumia njia hii unaweza kuzunguka mlima ukiwa juu.

•    Kufikia cave ya pili kuna njia panda unaweza kwenda Mawenzi na kukutana na watu waliopandia njia ya Marangu

•    Ukifika cave ya tatu unaenda moja kwa moja mpaka Kibo hut utakutana na watu waliopandia  njia ya Marangu.

•    Kwa njia hii unakutana na watu  waliopandia  njia ya Machame katika cave ya tatu kwa kupitia School hut kuelekea barafu

 Kaburi la Mangi Horombo

Kaburi hili lipo Tarafa ya Mengwe kata ya Mengeni takribani umbali wa mita sabini toka barabara kuu ya lami itokayo Moshi kwenda Tarakea. Kaburi hili lina mvuto wa kipekee kutokana na urefu wa Mangi Horombo ambaye alikuwa na urefu wa futi nane na inchi mbili (Futi 8.2”). Kimsingi linakumbusha historia ya Warombo kwa ujumla wake tangu alipofariki mwaka 1802.   

MAHANDAKI

Katika kumbukumbu ya vita kati ya Warombo na Wamasai, kuna mahandaki katika eneo la kijiji cha Mamsera Tarafa ya Mengwe lenye urefu wa mita 68 chini ya mlima Uwa. Katika handaki hilo lililotumiwa na watu kujificha lina vyumba ambayo vilitengwa kwa matumizi mbalimbali yakiwemo jiko, malazi sehemu ya kuwaficha watoto na vyumba kwa ajili ya walinzi.Handaki hilo liligundulika mwaka 2007 na mwananchi mmoja wa eneo hilo, hivyo tunakaribisha wananchi toka Ndani na Nje ya nchi kuja kuliona na kupata historia ya kabila la Warombo



Matangazo

  • MATOKEO YA USAHILI WA WALIOOMBA KAZI YA KUKUSANYA MAPATO NA KAZI YA USAFI August 27, 2024
  • TANGAZO LA UUZAJI WA VIWANJA VYA HALMASHAURI YA WILAYA YA ROMBO June 14, 2024
  • TANGAZO LA MNADA WA HADHARA August 26, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI YA AJIRA YA MKATABA July 16, 2024
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • KARIBU KWENYE BARAZA LA MADIWANI.

    May 07, 2025
  • KARIBU KWENYE BARAZA LA MADIWANI.

    May 07, 2025
  • ZAID YA SHILINGI MILIONI MIA SITA AROBAINI NA MOJA YA KABIDHIWA KWA VIKUNDI 52

    April 17, 2025
  • ZAID YA SHILINGI MILIONI MIA SITA AROBAINI NA MOJA YA KABIDHIWA KWA VIKUNDI 52

    April 17, 2025
  • Ona Zote

Video

Maafisa Elimu Kata wakizifanyia Majaribio Pikipiki
Video Zaidi

Viunganishi Vya Haraka

  • Muundo wa Halmashauri
  • Wasiliana Nasi Kwa
  • Miladi iliyokamilika

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • MFUMO WA TAUSI
  • Ffars
  • Tamisemi
  • Idara ya Takwimu (NBS)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Rombo District Council,Mkuu Bomani Street

    Sanduku la Posta: P.o Box 52,Mkuu,Rombo

    Simu: 027-2757101

    Simu ya Mkononi: 027-2757101

    Barua Pepe: ded@rombodc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright@2019Rombodc.all rights reserved