• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Halmashauri ya Wilaya ya Rombo
Halmashauri ya Wilaya ya Rombo

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali Za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Rombo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Ujenzi
      • Maji
      • Mipango na Takwimu
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Ardhi na Maliasili
      • Utumishi na Utawala
      • Afya
    • Kitengo
      • TEHAMA
      • Manunuzi na Ugavi
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Nyuki
      • Uchaguzi
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • maji
    • Elimu
    • Watumishi
    • Kilimo
    • Afya
    • Mifugo
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Mipya
  • Machapisho
    • Fomu
    • Sheria Ndogo
    • Ripoti
    • Taratibu
    • Taarifa za Fedha
      • Taarifa ya makisio ya Mapato
      • Taarifa ya Mapato Halisi
      • Taarifa ya Matumizi
      • MTEF
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Hotuba

Huduma ya Maji


Wilaya kupitia Idara ya Maji hushughulika na utekelezaji wa mipango ya muda mrefu na mfupi ya usambazaji wa maji katika maeneo ya mijini na vijijini ikishirikiana na kampuni inayosimamia huduma ya maji wilayani KILIWATER.

Huduma ya maji katika Wilaya ya Rombo inatolewa katika vijiji 68 kwa wakazi wapatao 260,963, wilaya ina vyanzo vya maji 30 kati ya hivyo vyanzo 29 ni vya maji ya mtiririko na vyanzo vitano (1) ni visima virefu.

Kiasi cha maji kinachozalishwa kwa siku ni mita za ujazo 27,000 kipindi cha masika na kwa kipindi cha kiangazi kiasi hicho hupungua na kufikia mita za ujazo 22,000, wakati mahitaji ya siku ni mita za ujazo 40,000. Mtandao wa mabomba unakadiriwa kufikia kilometa 1,300.

 Idaya ya Maji inatekeleza Programu ya Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RWSSP)

Lengo la utekelezaji wa programu hii ni kuwapatia wananchi huduma ya maji katika umbali usiozidi mita 400, au kutumia muda usiozidi dakika 30 kwenda kuchota maji na kurudi nyumbani. Kwenye awamu ya kwanza ya Utekelezaji wa Programu ya Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (Rural Water Supply and Sanitation Programme-RWSSP) kwa Vijiji kumi kwa wilaya ya Rombo ulihusisha kijiji cha Ngoyoni, Ngareni, Shimbi Mashariki, Ushiri, Mahorosha, Msaranga, Kahe, Leto, Kiraeni na Urauri.

 

Teknolojia iliyopendekezwa na wananchi chini ya ushauri wa wataalam ni uchimbaji wa visima virefu (Boreholes) kwa vijiji tisa na maji ya mtirirko kwa kijiji kimoja tu cha ushiri.

Uchimbaji wa visima hivyo ulifanywa na mkandarasi Water Solution Drilling Co.ltd chini ya usimamizi wa Mtaalam Mshauri Norplan Tz Ltd.

 Hali halisi ya utekelezaji wa Programu ya Maji na Usafi wa Mazingira vijijini

Uchimbaji wa visima virefu katika vijiji vya Kahe, Kiraeni, Mahorosha, Msaranga, Ngoyoni, Urauri, Shimbi-Mashariki, Leto na Ngareni ulikamilika, ambapo kati ya vijiji hivyo visima vilivyopata maji ya kutosha ni kijiji cha Kahe na Shimbi- Mashariki hivyo kuendelezwa kwa kujengewa miundombinu. Kwa vijiji vilivyochibwa visima virefu na kukosa maji( Dry borehole) ilitafutwa njia mbadala kwa kutoa maji kwenye bomba kubwa la maji toka vyanzo vya msitu wa Kinapa marangu.

Ujenzi wa miundombinu ya maji katika vijiji vya Mahorosha, Msaranga, Kiraeni na Ngoyoni umekamilika na wananchi wanapata huduma ya Maji.

Ujenzi wa miundombinu ya maji kwa vijiji vya Kahe na Ushiri imekamilika na huduma inaendelea kutolewa.

Miradi ya maji katika kijiji cha Shimbi – Masharaki, Ngareni na Leto wakandarasi walianza kazi mwezi Julai 2015. Katika vijiji vyote vitatu vyanzo vya maji ni visima virefu hivyo zitatumika pump (Pumped scheme).Miradi hii inatekelezwa kwa awamu.

Awamu ya Kwanza ilikuwa ujenzi wa:-

  • Matenki makubwa ya kuhifadia maji (75m3 na 150m3)
  • Matenki madogo kwa ajili ya kuhifadhia maji toka kwenye kisima (Samp tank) 25m3
  • Nyumba ya Pampu
  • Mtandao wa bomba ya njia kuu.(Raising main).

Awamu ya Pili ilikuwa ujenzi wa;

  • Mtandao wa kusambazia maji (Distribution network)
  • Ujenzi wa vituo vya kuchotea maji
  • Ujenzi wa Vivunja nguvu (Break Pressure tank)

Kwasasa wakandarasi wote wameshajenga matenki ya kuhifadhia maji yenye lita 150,000 kwa kijiji cha Shimbi Mashariki na Leto na lita 75,000 na 25,000 kwa kijiji cha Ngareni.Jumla ya vituo vya kuchotea maji 56 vimejengwa Wakandarasi wanaendelea na kazi za umaliziaji wa miradi hiyo.

Mafanikio

  1. Kukamilika kwa miradi katika vijiji 6 vya utekelezaji wa program ya maji na usafi wa mazingira katika vijiji kumi vya awamu ya I
  2. Upatikanaji wa maji kwa muda usiozidi nusu saa kutoka kwenye makazi ya watu

Mikakati

  1. Kuendelea kutenga fedha kwenye bajeti za kutekeleza miradi ya maji inayoendelea kutekelezwa.
  2. Kuanza usanifu wa kutumia umeme wa jua kwenye miradi ya maji


Matangazo

  • MATOKEO YA USAHILI WA WALIOOMBA KAZI YA KUKUSANYA MAPATO NA KAZI YA USAFI August 27, 2024
  • TANGAZO LA UUZAJI WA VIWANJA VYA HALMASHAURI YA WILAYA YA ROMBO June 14, 2024
  • TANGAZO LA MNADA WA HADHARA August 26, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI YA AJIRA YA MKATABA July 16, 2024
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • KARIBU KWENYE BARAZA LA MADIWANI.

    May 07, 2025
  • KARIBU KWENYE BARAZA LA MADIWANI.

    May 07, 2025
  • ZAID YA SHILINGI MILIONI MIA SITA AROBAINI NA MOJA YA KABIDHIWA KWA VIKUNDI 52

    April 17, 2025
  • ZAID YA SHILINGI MILIONI MIA SITA AROBAINI NA MOJA YA KABIDHIWA KWA VIKUNDI 52

    April 17, 2025
  • Ona Zote

Video

Maafisa Elimu Kata wakizifanyia Majaribio Pikipiki
Video Zaidi

Viunganishi Vya Haraka

  • Muundo wa Halmashauri
  • Wasiliana Nasi Kwa
  • Miladi iliyokamilika

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • MFUMO WA TAUSI
  • Ffars
  • Tamisemi
  • Idara ya Takwimu (NBS)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Rombo District Council,Mkuu Bomani Street

    Sanduku la Posta: P.o Box 52,Mkuu,Rombo

    Simu: 027-2757101

    Simu ya Mkononi: 027-2757101

    Barua Pepe: ded@rombodc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright@2019Rombodc.all rights reserved