• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Halmashauri ya Wilaya ya Rombo
Halmashauri ya Wilaya ya Rombo

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali Za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Rombo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Ujenzi
      • Maji
      • Mipango na Takwimu
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Ardhi na Maliasili
      • Utumishi na Utawala
      • Afya
    • Kitengo
      • TEHAMA
      • Manunuzi na Ugavi
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Nyuki
      • Uchaguzi
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • maji
    • Elimu
    • Watumishi
    • Kilimo
    • Afya
    • Mifugo
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Mipya
  • Machapisho
    • Fomu
    • Sheria Ndogo
    • Ripoti
    • Taratibu
    • Taarifa za Fedha
      • Taarifa ya makisio ya Mapato
      • Taarifa ya Mapato Halisi
      • Taarifa ya Matumizi
      • MTEF
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Hotuba

Kilimo

     Kilimo

Wilaya ya Rombo ina jumla ya Ha 44,114 zinazofaa kwa kilimo. Kati ya hizo Hekta 18,168 zinalimwa mazao ya kudumu (Migomba, kahawa) Eneo lililobakia linatumika kwa kilimo cha mazao ya msimu kama inavyoonekana kwenye jedwali hapa chini:

 Mazao yanayolimwa

    Aina ya Zao                          Eneo linalolimwa

 1    Kahawa na Migomba                15,950

 2    Migomba pekee (pure stand)     2000

 3    Kahawa peke (pure stand)         68

 4    Mahindi                                     12,000

 5    Maharage                                 6000

 6    Kunde                                       128

 7    Mbaazi                                      400

 8    Alizeti                                       900

 9    Karanga                                  450

 10    Magimbi                                 400

 11    Ulezi                                      1760

 12    Mtama                                     200

 13    Mhogo                                    670

 14    Viazi Mviringo                        2650

 15    Viazi vitamu                           200

 16    Choroko                                100

 17    Mboga                                   88

 18    Matunda                               150

       Jumla                                   44,114


 Hali ya hewa

Wilaya ya Rombo ina Misimu miwili ya mvua ambayo ni Vuli na Masika. Msimu wa Vuli huanza mwezi Oktoba hadi Desemba. Msimu huu ndio unaotegemewa zaidi na wakulima.

 Msimu wa Masika huanza mwezi Machi hadi Mei kila mwaka. Wilaya ina Kanda tatu (3) za kilimo ambazo ni Ukanda wa Juu, Ukanda wa Kati na Ukanda wa chini.

Ukanda wa juu upo kati ya mita 1,200 hadi mita 1,800 juu ya usawa wa bahari. Aina ya udongo inayopatikana katika Ukanda huu ni 'Volcanic soil' na Mazao yanayolimwa katika Ukanda huu ni kahawa, migomba na mahindi ya muda mrefu viazi mviringo, pamoja na mboga na matunda(parachichi). Pia sehemu kubwa ya Ukanda huu ni eneo la Msitu. Hali ya hewa katika Ukanda huu; mvua ni kati ya 1000mm hadi 1500mm na nyuzi joto 150C hadi 200 C. Ukanda huu una msongamano mkubwa wa watu (kaya 480-500 kwa kilomita moja ya eneo (/km2).


Ukanda wa kati upo kati ya mita 900m- 1,200 juu ya usawa wa bahari. Udongo uliopo katika ukanda huu ni mchanyiko wa mfinyanzi na mboji. Hali ya joto katika ukanda huu ni kati ya nyuzi joto 200-300 C, Mazao yanayolimwa katika Ukanda huu ni pamoja na kahawa, migomba, mahindi ya muda mfupi, mazao ya jamii zote za kunde, matunda hasa maembe, alizeti, Mhogo, Karanga na mtama.


Ukanda wa chini upo chini ya mita 900 juu ya usawa wa bahari.Hali ya hewa katika Ukanda huu  ni joto(250C -300C) pamoja na ukame wa mara kwa mara. Aina ya udongo katika ukanda huu ni udongo mchanganyiko (variable textures from sandy clay to loams).


 Hali ya kilimo/Agriculture potentials

Wakulima wengi bado wanatumia jembe la mkono kwenye kilimo chao kutokana na hali halisi ya mashamba yao kuwa madogo(kati ya 1/2  Ekari hadi Ekari1. Matumizi ya matrekta na wanyama kazi yapo kwa kiwango kidogo. Wakulima wameshauriwa kutumia zaidi matrekta madogo (power tillers) ambapo jumla ya matrekta madogo 14 yapo na yanafanya kazi katika maeneo mbalimbali ya wilaya. Trekta hizo zinamilikiwa na vikundi vilivyowezeshwa na Serikali, Taasisi na watu binafsi.  Kilimo chetu kinahitaji matumizi makubwa ya mbolea hasa samadi kutokana na mashamba kulimwa mfululizo bila kupumzishwa.Hii imetokana na kuwepo kwa misimu miwili ya mvua na udogo wa mashamba ambao unawalazimisha wakulima kulima kwa misimu yote miwili bila kupumzisha mashamba yao.

Kahawa bado ndio zao kuu la biashara la wilaya ya Rombo ambapo kati ya tani 2,000 hadi 3000 huvunwa kwa mwaka. Ndizi pamoja na kuwa zao la chakula lakini linachangia kwa kiasi kikubwa kipato cha wakulima. Uzalishaji wa ndizi uko juu kutokana na mbegu bora za migomba aina za williams, chinese cavendish na lacatan. Wastani wa tani 191,400 huzalishwa kila mwaka ambapo asilimia 70% huuzwa katika masoko mbalimbali ya ndani na nje ya wilaya na asilimia 30% hutumika kwa matumizi ya nyumbani (chakula).






Matangazo

  • MATOKEO YA USAHILI WA WALIOOMBA KAZI YA KUKUSANYA MAPATO NA KAZI YA USAFI August 27, 2024
  • TANGAZO LA UUZAJI WA VIWANJA VYA HALMASHAURI YA WILAYA YA ROMBO June 14, 2024
  • TANGAZO LA MNADA WA HADHARA August 26, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI YA AJIRA YA MKATABA July 16, 2024
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • KARIBU KWENYE BARAZA LA MADIWANI.

    May 07, 2025
  • KARIBU KWENYE BARAZA LA MADIWANI.

    May 07, 2025
  • ZAID YA SHILINGI MILIONI MIA SITA AROBAINI NA MOJA YA KABIDHIWA KWA VIKUNDI 52

    April 17, 2025
  • ZAID YA SHILINGI MILIONI MIA SITA AROBAINI NA MOJA YA KABIDHIWA KWA VIKUNDI 52

    April 17, 2025
  • Ona Zote

Video

Maafisa Elimu Kata wakizifanyia Majaribio Pikipiki
Video Zaidi

Viunganishi Vya Haraka

  • Muundo wa Halmashauri
  • Wasiliana Nasi Kwa
  • Miladi iliyokamilika

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • MFUMO WA TAUSI
  • Ffars
  • Tamisemi
  • Idara ya Takwimu (NBS)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Rombo District Council,Mkuu Bomani Street

    Sanduku la Posta: P.o Box 52,Mkuu,Rombo

    Simu: 027-2757101

    Simu ya Mkononi: 027-2757101

    Barua Pepe: ded@rombodc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright@2019Rombodc.all rights reserved