Uongozi wa Mkoa wa Kilimanjaro ukiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Nurdin Babu, Katibu Tawala wa Mkoa Tixon Nzunda Pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama Juni 1 wamefanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo katika Halamashauri ya Wilaya ya Rombo.
Ziara hiyo ililenga katika kuhakiki thamani ya miradi husika na kupata ripoti kamili kuhusu miradi hiyo. Jumla ya miradi nane ya maendeleo ilitembelewa ambapo baadhi ilionekana kuwa na dosari.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro Tixon Nzunda ametoa wito kwa Mkurugenzi wa Halmashauri pamoja na Wakuu wa Idara kuhakikisha wanazitafutia ufumbuzi changamoto hizo ndani ya siku saba. Pia amesisitiza upatikanaji wa taarifa kamili za kila mradi kuanzia siku mradi ulipoanza hadi ulipifikia pamoja na majibu ya vipimo vya material yote yaliyotumika kuambatishwa na kuagiza taarifa hizo zitumwe mkoani ndani ya siku saba.
Aidha, Bw. Nzunda aliwasisitiza wajumbe juu ya uwajibikaji katika kutekeleza majukumu yao hususani yale yanayohusu miradi ya maendeleo na kuwaeleza kuwa endapo atabaini tena dosari na uzembe wa aina yoyoye katika miradi hiyo basi hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa wahusika .
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Rombo Mhe. Kanali Hamisi Maiga aliushukuru uongozi wa Mkoa kwa kufika katika Wilaya yake na kuahidi kufanyiwa kazi kwa changamoto zote zilizojitokeza kwa kushirikiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halamsashauri.
Cc. Afisa Mawasiliano na Uhusiano Serikalini
Rombo District Council,Mkuu Bomani Street
Sanduku la Posta: P.o Box 52,Mkuu,Rombo
simu: 027-2757101
Mobile: 027-2757101
staff mail: ded@rombodc.go.tz
Copyright@2019Rombodc.all rights reserved