FURSA ZA UTALII
Katika Wilaya kuna maeneo mbalimbali ambayo ni vivutio vya utalii. Maeneo hayo ni pamoja na Ziwa Chala, Vilele vya Mlima Kilimanjaro (Mawenzi na Kibo), Kaburi la Mangi Horombo na Mahandaki yaliyotumika kama maeneo ya maficho wakati wa Vita.
Ziwa Chala
Ziwa hili lipo mpakani mwa Nchi ya Kenya na Tanzania takribani kilomita 45 kutoka barabara ya Moshi- Taveta; kwa kuingilia eneo la Holili
Ziwa Chala lilitokana na mlipuko wa volkano ambalo limedidimia kwa muonekano. Ziwa hili linasemekana kuwa na muunganiko wa kijiolojia na mlima Kilimanjaro. Ziwa lina takribani kina cha mita 3,000 ambapo hadi sasa hakuna utafiti wa kisanyansi unaothibitisha urefu wa kina cha ziwa hili ambalo lina mvuto wa kipekee kwani hakuna mto unaoingiza, wala kutoa maji. Ni ziwa lenye maji baridi na samaki wa maji baridi.
Eneo la Ziwa Chala, kuna hekta zipatazo 23(ishirini na tatu) kwa upande wa Tanzania ambazo ni mashamba yanayomilikiwa na watu binafsi eneo hili linaweza kutumika katika ujenzi wa mahoteli na “campsite”.
Aidha tunahita wananchi wa Ndani na Nje ya Nchi ili waje kufanya utalii kwa kujionea maajabu ya umbile la ziwa hilo. Huduma za Hoteli zinapatikana kwa kuwa limepakana na hoteli ya kitalii inayojulikana kwa jina la lake Chala safari Lodge.
Vilele vya Mlima Kilimanjaro
Vilele vya mlima huu vinapatikana Wilaya ya Rombo. Njia inayotumika kupandia mlima Kilimanjaro ambayo ipo Rombo inajulikana kwa jina la Nalemuru route. Ili kufika njia hii ni km. 95 toka Moshi Mjini. Njia hii inapitika kwa urahisi na ina vivutio vya wanyama mfano Mbega, Tembo, Nyani, Kima, Tumbili, Ng’edere, Ngiri, Simba wachache, Mbwa mwitu, Mbweha na Wanyama wengine.
Kuna vituo vitatu kwa kupitia njia hii:-
1. Simba Camp 2ndcave 3rdcave Kibo halfSummit
2. Samba Camp 2nd cave Kikelelwa cave Mawenzi half Kibo half Summit
3. Samba cave 2nd cave 3rd cave School half Barafu Summit
• Ni njia rahisi kuliko zote za kupandia Mlima Kilimanjaro, haina mwinuko sana ni njia ambayo ukiwa unapanda unaweza kuona Mbuga ya wanyama Amboseli iliyopo Kenya na Wilaya ya Kajiado kwa urahisi. Wakati unapanda unatumia siku tano (5) kupanda mlima huu. Kwa njia ya Marangu unaweza kutumia siku (6 – 7)
• Kwa njia hii utapanda na kushukia Marangu, vile vile kwa kutumia njia hii unaweza kuzunguka mlima ukiwa juu.
• Kufikia cave ya pili kuna njia panda unaweza kwenda Mawenzi na kukutana na watu waliopandia njia ya Marangu
• Ukifika cave ya tatu unaenda moja kwa moja mpaka Kibo hut utakutana na watu waliopandia njia ya Marangu.
• Kwa njia hii unakutana na watu waliopandia njia ya Machame katika cave ya tatu kwa kupitia School hut kuelekea barafu
Kaburi la Mangi Horombo
Kaburi hili lipo Tarafa ya Mengwe kata ya Mengeni takribani umbali wa mita sabini toka barabara kuu ya lami itokayo Moshi kwenda Tarakea. Kaburi hili lina mvuto wa kipekee kutokana na urefu wa Mangi Horombo ambaye alikuwa na urefu wa futi nane na inchi mbili (Futi 8.2”). Kimsingi linakumbusha historia ya Warombo kwa ujumla wake tangu alipofariki mwaka 1802.
MAHANDAKI
Katika kumbukumbu ya vita kati ya Warombo na Wamasai, kuna mahandaki katika eneo la kijiji cha Mamsera Tarafa ya Mengwe lenye urefu wa mita 68 chini ya mlima Uwa. Katika handaki hilo lililotumiwa na watu kujificha lina vyumba ambayo vilitengwa kwa matumizi mbalimbali yakiwemo jiko, malazi sehemu ya kuwaficha watoto na vyumba kwa ajili ya walinzi.Handaki hilo liligundulika mwaka 2007 na mwananchi mmoja wa eneo hilo, hivyo tunakaribisha wananchi toka Ndani na Nje ya nchi kuja kuliona na kupata historia ya kabila la Warombo
Rombo District Council,Mkuu Bomani Street
Sanduku la Posta: P.o Box 52,Mkuu,Rombo
simu: 027-2757101
Mobile: 027-2757101
staff mail: ded@rombodc.go.tz
Copyright@2019Rombodc.all rights reserved