Maadhimisho ya siku ya wazee duniani hufanyika kila mwaka tarehe moja oktoba.Katika wilaya ya Rombo Maadhimisho haya yamefanyika leo tarehe 02/10/2023 katika ukumbi wa Halmashauri. Washiriki walikuwa Wazee kutoka sehemu mbalimbali ndani ya Wilaya ya Rombo.
Mgeni Rasmi katika Maadhimisho haya alikua ni Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Rombo Dr. Elionora Shayo.
Pia, Wataalamu mbalimbali kutoka Idara ya Afya Ustawi wa Jamii na Lishe ngazi ya Wilaya walishiriki kutoa Elimu pamoja na upimaji wa Afya ambapo shughuli zilizofanyika ni:
Kutoa Ushauri Nasaha kwa Waze
Kupima Afya bure ambapo wazee wote waliofika walipimwa magonjwa ya Shinikizo la Damu, Kisukari na Macho.
Kutoa Elimu ya Lishe, Chanjo Ukatili wa Kijinsia na Ukatili dhidi ya Watoto.
Rombo District Council,Mkuu Bomani Street
Sanduku la Posta: P.o Box 52,Mkuu,Rombo
simu: 027-2757101
Mobile: 027-2757101
staff mail: ded@rombodc.go.tz
Copyright@2019Rombodc.all rights reserved