• Contact us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaint |
Halmashauri ya Wilaya ya Rombo
Halmashauri ya Wilaya ya Rombo

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Rombo District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • ujenzi
      • maji
      • Planning and Statitics
      • Livestock and Fishing
      • Community DEvelopment
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Elimu Msingi
      • Ellimu Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Land and natural Resources
      • Human Resource and Administration
      • Health
    • Unit
      • ICT
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Law
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
    • Organisation Structure
  • Investiment Opportunities
    • Vivutio vya utalii
    • Industry
  • Our Services
    • Water
    • Elimu
    • Watumishi
    • Kilimo
    • Health
    • Mifugo
  • Councillors
    • List of Councillors
    • Permanent Commitees
    • Scheduals of Legal sessions
  • Projects
    • Completed projects
    • Ongoing projects
    • New Project
  • Publications
    • Forms
    • Acts
    • Report
    • Taratibu
    • Taarifa za Fedha
      • Taarifa ya makisio ya Mapato
      • Taarifa ya Mapato Halisi
      • Taarifa ya Matumizi
      • MTEF
    • Guidelines
  • Media Centre
    • Videos
    • News
    • Press Releae
    • Photo Gallery
    • Speech

Wawili waswekwa rumande kusuasua miradi ya maji Rombo

Posted on: January 24th, 2020

Watu wawili,Godson Josea -Msimamizi wa mradi wa maji wa Shimbi Mashariki na Mhandisi Amos Thomas walio chini ya Mkandarasi  HECO SANMARK (T) LTD  wanashikiliwa na jeshi la polisi  mpaka Mkandarasi huyo atakapojisalimisha kwenye uongozi wa wilaya.

Maamuzi hayo yamefanywa na Naibu waziri wa Maji Jumaa Aweso baada ya kufika katika mradi wa maji Shimbi Mashariki na kukuta mradi ulioanza toka mwaka 2013 haujakamilika na mkandarasi  ambaye amekwishalipwa fedha na serikali kiasi cha shilingi milioni 100 hayupo eneo la mradi, huku kukiwa na malalamiko ya vibarua kutokulipwa fedha zao.

Aidha Naibu Waziri Aweso amemuagiza Mhandisi wa RUWASA Joseph Mcharo  kuhakikisha anafuata taratibu za kisheria  na kuvunja mkataba na HECO SANMARK (T) LTD  pindi atakapojisalimisha  ili asilimia 12 zilizobaki za mradi kukamilika zifanywe na wataalamu wa Wakala wa Usambazaji Maji na Usafi Wa Mazingira (RUWASA)Wilaya ya  Rombo  .

Ameongeza kuwa mbali na kushughulikia suala la vibarua kulipwa fedha zao , pia RUWASA wanatakiwa kuhakikisha mzabuni wa  pampu za maji analipwa fedha yake na pampu ziwashwe ili wananchi wa eneo hilo wapate huduma maji.

Mhandisi  Mcharo  amesema kuwa mradi wa maji Shimbi Mashariki wenye thamani ya shilingi milioni 887.4 umeshatekelezwa kwa asilimia 88 huku Mkandarasi akiwa amekwishalipwa kiasi cha zaidi ya milioni 400 na anadai kiasi cha shilingi milioni 86 tu.

Amesema sababu kubwa wanayoitoa wakandarasi ya kuchelewa kukamilisha miradi ni kutolipwa madai yao kwa wakati , na pindi wanapoandikia madai yao wanasimamisha ujenzi mpaka walipwe fedha zao ndio waendelee na kazi.

Vilevile Naibu Waziri Aweso  alitembelea mradi wa maji katika kijiji cha  Leto wenye thamani ya shilingi milioni 927.9 ambao nao pia haujakamilika kitu kinachosababisha wanakijiji wa eneo hilo kwenda kuchota maji nchi jirani ya Kenya.


Matangazo

  • MATOKEO YA USAHILI WA WALIOOMBA KAZI YA KUKUSANYA MAPATO NA KAZI YA USAFI August 27, 2024
  • TANGAZO LA UUZAJI WA VIWANJA VYA HALMASHAURI YA WILAYA YA ROMBO June 14, 2024
  • TANGAZO LA MNADA WA HADHARA August 26, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI YA AJIRA YA MKATABA July 16, 2024
  • View All

Habari Mpya

  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI.

    May 29, 2025
  • KARIBU KWENYE BARAZA LA MADIWANI.

    May 07, 2025
  • KARIBU KWENYE BARAZA LA MADIWANI.

    May 07, 2025
  • ZAID YA SHILINGI MILIONI MIA SITA AROBAINI NA MOJA YA KABIDHIWA KWA VIKUNDI 52

    April 17, 2025
  • View All

Videos

Maafisa Elimu Kata wakizifanyia Majaribio Pikipiki
More Videos

Kurasa za haraka

  • Muundo wa Halmashauri
  • Wasiliana Nasi Kwa
  • Miladi iliyokamilika

Kurasa za karibu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • MFUMO WA TAUSI
  • Ffars
  • Tamisemi
  • Idara ya Takwimu (NBS)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact us

    Rombo District Council,Mkuu Bomani Street

    Sanduku la Posta: P.o Box 52,Mkuu,Rombo

    simu: 027-2757101

    Mobile: 027-2757101

    staff mail: ded@rombodc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Sitemap

Copyright@2019Rombodc.all rights reserved