• Contact us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaint |
Halmashauri ya Wilaya ya Rombo
Halmashauri ya Wilaya ya Rombo

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Rombo District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • ujenzi
      • maji
      • Planning and Statitics
      • Livestock and Fishing
      • Community DEvelopment
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Elimu Msingi
      • Ellimu Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Land and natural Resources
      • Human Resource and Administration
      • Health
    • Unit
      • ICT
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Law
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
    • Organisation Structure
  • Investiment Opportunities
    • Vivutio vya utalii
    • Industry
  • Our Services
    • Water
    • Elimu
    • Watumishi
    • Kilimo
    • Health
    • Mifugo
  • Councillors
    • List of Councillors
    • Permanent Commitees
    • Scheduals of Legal sessions
  • Projects
    • Completed projects
    • Ongoing projects
    • New Project
  • Publications
    • Forms
    • Acts
    • Report
    • Taratibu
    • Taarifa za Fedha
      • Taarifa ya makisio ya Mapato
      • Taarifa ya Mapato Halisi
      • Taarifa ya Matumizi
      • MTEF
    • Guidelines
  • Media Centre
    • Videos
    • News
    • Press Releae
    • Photo Gallery
    • Speech

Wanaume na Hofu ya Kupima VVU

Posted on: September 26th, 2018

Uzinduzi wa kampeni  ya Pima, Jitambue, Ishi  Wilaya ya Rombo ulifanyika  siku ya tarehe 25.09.2018 katika viwanja vya stendi ya mabasi Mkuu ikiwa ni kampeni ya Kitaifa yenye lengo la kufikia asilimia 90 ya watanzania ambao wamepimwa  VVU na kujua hali zao ifikapo mwaka 2020 na kundi la kwanza linalolengwa ni wanaume, likifuatiwa na vijana wa kike kuanzia miaka 15 hadi 25 na kundi la tatu ni wanawake wajawazito.

Katika uzinduzi huo Mkuu wa Wilaya ya Rombo, Mhe.  Agnes Hokororo amewaomba wanaume wa Rombo kujitokeza kwa wingi na kupima  hali zao na kuacha kuwategea wake zao kwasababu ni muhimu katika familia au kaya zetu kuhakikisha kila mmoja wetu ametambua afya yake .

“Takwimu za kitaifa zinaonesha wanaume wamekuwa na muitikio mdogo wa kupima VVU na kuwaachia wanawake hasa  wakinamama  wajawazito jukumu la kupima afya zao na wanapokutwa hawana maambukizi  na wao wanajihakikishia kuwa wako salama kupitia vipimo vya wake zao.” Alisema Hokororo

Aliongeza kuwa kuna faida kubwa ya kujua hali ya afya zetu na iwapo ukikutwa na maambukizi kuanza dawa mapema ni mwili kuweza kupambana na virusi vinavyosababisha UKIMWI  na kufubaa mapema hatimaye kupunguza kiwango cha virusi mwilini.

“Ninachukua fursa hii kuishukuru serikali chini ya Wizara ya Afya, Jinsia , Wazee na Watoto  kwa kubuni na kufanya kampeni hii lakini pia nichukue fursa hii kuwaomba sana viongozi wa dini mbalimbali kusaidia kushawishi waumini wao kupima afya ili kufahamu hali zao”, alimalizia Hokororo

Naye Mratibu wa UKIMWI  Wilaya ya Rombo Dkt Agripina Masao alisema kuwa zoezi la upimaji la kitaifa lenye kauli mbiu ya “Furaha yangu; Pima, Jitambue, Ishi” litaendelea mpaka novemba 30 mwaka huu ambapo kiwilaya tumepewa malengo ya kuhakikisha  tumepima watu 6,689.

Ameongeza kuwa zoezi hili lilianza toka tarehe 17 Septemba  na mpaka tarehe 23 Septemba watu 236 walijitokeza kupima na hakuna na aliyekutwa na maambukizi  na zoezi litaendelea kufanyika mpaka Novemba  30 , 2018 kwenye Vituo vya Afya, Zahanati na Hospitali zote zinazotoa huduma ya kupima VVU.

Lengo kuu la kampeni hii ya kitaifa ni kutekeleza mikakati ya kufikia 90 tatu yaani 909090 ifikapo mwaka 2020, 90 ya kwanza ikiwakilisha asilimia ya watu watakaojitokeza kupima VVU na kujua hali zao za maambukizi, 90 ya pili ni asilimia ya watu waliokutwa na maambukizi na kuanza dawa mara moja, 90 ya tatu ni asilimia ya watu wanaotumia dawa kwa uaminifu ili waweze kuwa na kiwango kidogo cha Virusi Vya UKIMWI.





Matangazo

  • MATOKEO YA USAHILI WA WALIOOMBA KAZI YA KUKUSANYA MAPATO NA KAZI YA USAFI August 27, 2024
  • TANGAZO LA UUZAJI WA VIWANJA VYA HALMASHAURI YA WILAYA YA ROMBO June 14, 2024
  • TANGAZO LA MNADA WA HADHARA August 26, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI YA AJIRA YA MKATABA July 16, 2024
  • View All

Habari Mpya

  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI.

    May 29, 2025
  • KARIBU KWENYE BARAZA LA MADIWANI.

    May 07, 2025
  • KARIBU KWENYE BARAZA LA MADIWANI.

    May 07, 2025
  • ZAID YA SHILINGI MILIONI MIA SITA AROBAINI NA MOJA YA KABIDHIWA KWA VIKUNDI 52

    April 17, 2025
  • View All

Videos

Maafisa Elimu Kata wakizifanyia Majaribio Pikipiki
More Videos

Kurasa za haraka

  • Muundo wa Halmashauri
  • Wasiliana Nasi Kwa
  • Miladi iliyokamilika

Kurasa za karibu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • MFUMO WA TAUSI
  • Ffars
  • Tamisemi
  • Idara ya Takwimu (NBS)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact us

    Rombo District Council,Mkuu Bomani Street

    Sanduku la Posta: P.o Box 52,Mkuu,Rombo

    simu: 027-2757101

    Mobile: 027-2757101

    staff mail: ded@rombodc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Sitemap

Copyright@2019Rombodc.all rights reserved