• Contact us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaint |
Halmashauri ya Wilaya ya Rombo
Halmashauri ya Wilaya ya Rombo

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Rombo District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • ujenzi
      • maji
      • Planning and Statitics
      • Livestock and Fishing
      • Community DEvelopment
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Elimu Msingi
      • Ellimu Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Land and natural Resources
      • Human Resource and Administration
      • Health
    • Unit
      • ICT
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Law
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
    • Organisation Structure
  • Investiment Opportunities
    • Vivutio vya utalii
    • Industry
  • Our Services
    • Water
    • Elimu
    • Watumishi
    • Kilimo
    • Health
    • Mifugo
  • Councillors
    • List of Councillors
    • Permanent Commitees
    • Scheduals of Legal sessions
  • Projects
    • Completed projects
    • Ongoing projects
    • New Project
  • Publications
    • Forms
    • Acts
    • Report
    • Taratibu
    • Taarifa za Fedha
      • Taarifa ya makisio ya Mapato
      • Taarifa ya Mapato Halisi
      • Taarifa ya Matumizi
      • MTEF
    • Guidelines
  • Media Centre
    • Videos
    • News
    • Press Releae
    • Photo Gallery
    • Speech

Wananchi waridhia kulipa madeni ya wazabuni

Posted on: June 14th, 2019

Wananchi wa vijiji vya Katangara na Mrere wameridhia kuchangia deni la wazabuni kiasi cha shilingi milioni 23,744,000.00 ambalo limetokana na kukopa vifaa vya ujenzi wa maabara ya kisasa ya baiolojia na fizikia katika shule ya sekondari Mashati.

Maamuzi hayo yalifikiwa baada ya wataalamu kutoka ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji  ambao ni Afisa Mipango, Mkaguzi wa ndani, Mwanasheria pamoja na Afisa Elimu sekondari  kufanya mkutano na wananchi wa vijiji hivyo wakishirikiana na bodi ya shule, kamati ya ujenzi ya shule  pamoja na uongozi  wa vijiji na kujadili namna ya kulipa deni la mzabuni  ambaye amepeleka kesi mahakamani ili kulipwa deni lake.

Baada ya wananchi kusomewa taarifa kamili ya mradi na madeni ambayo mradi huo unadaiwa, wananchi waliridhia kulipa deni hilo kidogo kidogo kwa awamu kwa  kila kaya kuchangia shilingi elfu thelathini(30,000) kwa kuanza na zile kaya ambazo hazijachanga kabisa kwa uwiano wa shilingi 15,780,000 kijiji cha Mrere na shilingi 8,000,000.00 kijiji cha katangara ili kulipa deni lote ambalo mradi huo  unadaiwa.

Aidha  mradi wa maabara ya Mashati sekondari ni mradi ambao ulikataliwa kuzinduliwa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge mwaka jana kutokana na mzabuni kutokulipwa deni lake ,na  kumuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Rombo kuhakikisha anamlipa mzabuni aliyetoa vifaa vya ujenzi ndugu Sabas Shirima kiasi cha shilingi milioni 22,744,000.00 ambapo kiasi cha shilingi milioni kumi (10,000,000) kililipwa na halmashauri na kiasi kilichobaki kilitakiwa kulipwa kutokana na michango ya wananchi.

Hata hivyo baada ya Ofisi ya Mkurugenzi kulipa kiasi alichotakiwa kulipa bado upande wa wananchi hakuna malipo yeyote yaliyofanyika kitu kilichopelekea mdai kurudi mahakamani ili kukazia hukumu  ili amaliziwe deni lake lote, hatua ambayo ilibidi Mkurugenzi Mtendaji Bi Magreth L John na timu ya wataalamu kujipanga upya kwenda kuzungumza na wananchi wa vijiji hivyo.

Katika mkutano huo  wananchi  waliridhia kulipa deni hilo lililobaki kiasi cha shilingi milioni 12,744,000.00 la ndugu Sabas Shirima lakini pia walikubaliana walipe madeni yote ya mradi huo wanaodaiwa na wazabuni pamoja na mafundi ili kuepuka usumbufu, ambapo jumla ya deni  ambalo mradi huo unadaiwa ni shilingi 23,744,000.00

 

Matangazo

  • MATOKEO YA USAHILI WA WALIOOMBA KAZI YA KUKUSANYA MAPATO NA KAZI YA USAFI August 27, 2024
  • TANGAZO LA UUZAJI WA VIWANJA VYA HALMASHAURI YA WILAYA YA ROMBO June 14, 2024
  • TANGAZO LA MNADA WA HADHARA August 26, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI YA AJIRA YA MKATABA July 16, 2024
  • View All

Habari Mpya

  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI.

    May 29, 2025
  • KARIBU KWENYE BARAZA LA MADIWANI.

    May 07, 2025
  • KARIBU KWENYE BARAZA LA MADIWANI.

    May 07, 2025
  • ZAID YA SHILINGI MILIONI MIA SITA AROBAINI NA MOJA YA KABIDHIWA KWA VIKUNDI 52

    April 17, 2025
  • View All

Videos

Maafisa Elimu Kata wakizifanyia Majaribio Pikipiki
More Videos

Kurasa za haraka

  • Muundo wa Halmashauri
  • Wasiliana Nasi Kwa
  • Miladi iliyokamilika

Kurasa za karibu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • MFUMO WA TAUSI
  • Ffars
  • Tamisemi
  • Idara ya Takwimu (NBS)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact us

    Rombo District Council,Mkuu Bomani Street

    Sanduku la Posta: P.o Box 52,Mkuu,Rombo

    simu: 027-2757101

    Mobile: 027-2757101

    staff mail: ded@rombodc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Sitemap

Copyright@2019Rombodc.all rights reserved