Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Dkt AveMaria Semakafu (waliokaa katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na wahitimu wa chuo cha FDC Mamtukuna kushoto kwake ni Rigamba Mwita kaimu mkuu wa Chuo na Kulia ni Magreth John Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Rombo
Dkt AveMaria Semakafu Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia amesema vyuo vyote vya maendeleo ya wananchi (VMW) maarufu kama FDC(Folk Development College) ambavyo vyeti vyake vilikuwa havitambuliki na NACTE mchakato unaendelea na hivi karibuni vyuo hivyo vitaanza kutoa Tuzo zinazotambuliwa na NACTE.
Akizungumza katika mahafali ya 30 ya Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Mamtukuna Dkt Semakafu amesema kuwa vyuo vya FDC vimerithiwa na kuwa chini ya wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia toka mwezi wa pili mwaka jana na ahadi ni kuwa kabla ya mwaka mpya wa masomo kuanza, Tuzo halali zitakuwa zimepatikana na hata kwa wale waliokwishahitimu zitafanyiwa ulinganifu ili vyeti vyao viweze kupatiwa tuzo zinazotambulika.
“Ukishoka ndani ya Wizara haukubaliki na maelekezo yamekwishatolewa kwa NACTE na wameshawasilisha andiko la kwanza na muda si mrefu Wizara itakutana nao kupokea wasilisho , ili vyeti vinavyotolewa na vyuo vyote vya FDC vipewe tuzo inayotambulika na kuwarahisishia wahitimu kujiendeleza mpaka hatua ya shahada”, alisema Semakafu
Naye kaimu mkuu wa chuo cha maendeleo ya wananchi mamtukuna ndg Rigamba Mwita aliwasilisha changamoto ya uhaba wa wakufunzi katika baadhi ya fani kama vile fani ya uchoraji hivyo kuomba wizara iwasaidie kutatua changamoto hiyo.
Akijibu hoja hiyo Dkt Semakafu amesema kuwa wizara imejizatiti chini ya kurugenzi ya ufundi yenye kurugenzi saidizi inayoshughulika na FDC pekee, tayari wameshaona upungufu uliopo wa wakufunzi kulingana na fani zilizopo na linafanyiwa kazi na kushughulikiwa hatua kwa hatua.
Mpaka sasa jumla ya vyuo 54 vya FDC vipo chini ya Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia , pamoja na TTC 35, wadhibiti ubora kila wilaya, wadhibiti ubora kanda na wizarani.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Dkt AveMaria Semakafu akitoka eneo la mahafali huku akicheza mziki wa furaha
Rombo District Council,Mkuu Bomani Street
Sanduku la Posta: P.o Box 52,Mkuu,Rombo
simu: 027-2757101
Mobile: 027-2757101
staff mail: ded@rombodc.go.tz
Copyright@2019Rombodc.all rights reserved