Nia ya serikali ya kufikisha umeme katika kila kijiji imeshatimia katika wilaya ya Rombo ambapo mpaka sasa asilimia mia moja (100%) ya kata zote na vijiji vyake vimeshaguswa na umeme.
Hayo yamezungumzwa na Meneja wa TANESCO wilaya ya Rombo Eng. Hassan Lumuli katika kikao cha baraza la madiwani tarehe 8 Novemba 2019 kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya wilaya.
Aidha ameeleza kuwa kwa kipindi cha kuanzia Januari hadi Oktoba 31, mwaka huu , jumla ya wananchi 2,842 wameunganishiwa na huduma hiyo ,huku jumla kuu mpaka kufikia Oktoba 31,2019 wananchi 25,346 wameunganishiwa umeme , ikiwa ni idadi ya nyumba/kaya zilizounganishwa.
Pamoja na hilo ameliambia baraza kuwa wananchi ambao bado hawajaunganishiwa umeme, wanaweza kuunganishwa na huduma hiyo kwa bei elekezi ya serikali ya shilingi 27000 tu kwa maeneo ya vijijini.
Katika hatua nyingine Eng. Lumuli ametoa rai kwa wananchi kutokuwa na hofu ya kufungua viwanda kwa sababu TANESCO Rombo bado ina uwezo wa kuwahudumia , ikiwa na kiasi Megawatt 1.5 za umeme ambao hauna matumizi ,ambapo Matumizi makubwa ya umeme katika Wilaya ya Rombo ni Megawat 3.0, lakini Uwezo wa line ya kulisha umeme ni Megawat 4.5.
Rombo District Council,Mkuu Bomani Street
Sanduku la Posta: P.o Box 52,Mkuu,Rombo
simu: 027-2757101
Mobile: 027-2757101
staff mail: ded@rombodc.go.tz
Copyright@2019Rombodc.all rights reserved