Picha kwa hisani ya Mtandao
Vita dhidi ya janga la UKIMWI inajumuisha kupima ili kujua hali ya afya yako, kujihadhari na maambukizi, pamoja na kutumia dawa za kupunguza makali ya Virusi vya UKIMWI na UKIMWI bado inaendelea huku watu wengi hawataki kupima afya zao, wanakimbia majibu na wengine wanatoroka huduma za dawa.
Harakati za kupambana na gonjwa la UKIMWI wilayani Rombo zinaendelea kupitia huduma mbalimbali zinazotolewa katika vituo 41 vinavyotoa huduma za upimaji, vikiwemo vituo 7 vinavyotoa huduma za dawa za kupunguza makali ya UKIMWI, Hospitali 2,Vituo vya Afya 4 na Zahanati 1.
Hata hivyo takwimu zinaonesha kuwa watu wenye umri kati ya miaka 25-49 ndio wanaopata zaidi maambukizi ya virusi vya UKIMWI,ambapo katika kipindi cha April-June kati ya wanaume 207 waliopima kwa hiyari wanne(4) walikutwa na maambukizi na wanawake sita(6) kati ya 254 .
Kwa upande wa waliopima kwa ushawishi wanaume 16 kati ya 442 walikutwa na maambukizi na wanawake 32 kati ya 796, wanawake wajawazito waliopimwa ni 1583 na 13 walikutwa na maambukizi sawa na asilimia 0.8
Hali halisi ya wateja walioorodheshwa toka huduma ilipoanza mwaka 2005 mpaka june 2018 ni 6104, Katika kipindi cha April-June 2018 waliopata huduma ni 2844,walioko kwenye dawa ni 2833,wateja wapya walioandikishwa ni 107, walionzishiwa dawa ni 108, waliotoroka huduma ni 77 na waliofariki ni 28.
Kamati ya ya kudhibiti UKIMWI wilaya ya Rombo imeagiza taasisi na Asasi zote zinazojishughulisha na shughuli za kupambana na UKIMWI kuhakikisha zinaandaa taarifa zao za utekelezaji wa shughuli wanazozifanya na kuziwasilisha kwenye kikao.
Rombo District Council,Mkuu Bomani Street
Sanduku la Posta: P.o Box 52,Mkuu,Rombo
simu: 027-2757101
Mobile: 027-2757101
staff mail: ded@rombodc.go.tz
Copyright@2019Rombodc.all rights reserved