Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Rombo katika kijiji cha Kiwanda kata ya Kirongo Samanga utasaidia kuboresha miundombinu muhimu na kwa haraka kutokana na umuhimu wake katika ujenzi wa Hospitali ikiwa ni pamoja na maji, umeme na barabara.
Kamati ya ulinzi na usalama wilaya ikiongozwa na Mhe Mkuu wa wilaya , Mkurugenzi Mtendaji na timu yake pamoja na Waheshimiwa Madiwani wakiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri walifanya mkutano na wananchi wa kata hiyo katika kijiji cha kiwanda kwa lengo la kusikiliza kero zao na kuwapa taarifa rasmi ya ujenzi wa hospitali ya wilaya katika kijiji hicho.
Katika mawasilisho ya kero na mahitaji yaliyoombwa kwa wingi na wananchi ni shida ya maji, umeme, shule ya msingi, ujenzi wa kituo cha polisi uliosimama kwa muda mrefu. Pamoja na hayo pia waliridhia na kushukuru ujenzi wa Hospitali ya wilaya katika kijiji hiko kwani walikuwa wanatembea umbali mrefu kufuata huduma za afya.
Mkuu wa wilaya ya Rombo Mhe.Agnes Hokororo akizungumza na wananchi wa kirongo samanga aliwahakikishia maji lazima yafike kirongo samanga hasa kiwanda, japo kulikuwa na mpango wa muda mrefu wa kuleta maji kutoka ziwa Chala lakini kutokana na dharura ya ujenzi wa hospitali chanzo kingine cha kinyasini kilichopo katika hifadhi ya Kinapa kitatumika na tayari vibali vimeshatolewa hivyo taratibu za kuleta maji Kiwanda zimeshaanza.
Miundombinu mingine ambayo Mhe.Hokororo aliiongelea itakayoambatana na ujenzi wa hospitali ni pamoja na barabara ambazo ni lazima ziwepo kwa ajili ya magari ya wagonjwa na wananchi kuingia na kutoka Hospitali, umeme pia ni muhimu katika hospitali lakini pia wananchi wanatakiwa kujiorodhesha katika sehemu zenye kaya zaidi ya 10 ili waweze kupata nishati hiyo muhimu.
Ombi la ujenzi wa shule ya msingi na umaliziaji wa kituo cha polisi lilichukuliwa na kuahidiwa kufanyiwa kazi na kutokana na umuhimu wa huduma hizo, zitatekelezeka.
Rombo District Council,Mkuu Bomani Street
Sanduku la Posta: P.o Box 52,Mkuu,Rombo
simu: 027-2757101
Mobile: 027-2757101
staff mail: ded@rombodc.go.tz
Copyright@2019Rombodc.all rights reserved