Mhe.Mkuu wa Wilaya ya Rombo Agnes Hokororo(Kulia) akipokea Mwenge wa Uhuru Kutoka kwa Mhe.Mkuu wa Wilaya ya Siha Onesmo Buswelu(Kushoto)
Mwenge wa uhuru 2018 umepokelewa wilaya ya Rombo tarehe 30 Septemba na kufanikiwa kutembelea, kufungua, kuzindua na kuweka mawe ya msingi katika miradi ya maendeleo yenye thamani ya fedha za kitanzania Sh.1,359,419,048.70 ambapo kati ya miradi iliyozinduliwa ni kikundi cha kupambana na madawa ya kulevya shule ya sekondari Tarakea.
Akizindua kikundi hicho, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Mhandisi Charles Francis Kabeho aliridhishwa na ufahamu mpana waliouonesha vijana hao juu ya madawa ya kulevya, visababishi vya kutumia madawa pamoja na athari zake.
“Ninachukua fursa hii kuwapongeza vijana hawa wanafunzi, kwa kuhakikisha wanakuwa na kikundi cha kuendesha mapambano dhidi ya dawa za kulevya, vijana wameiva, wamefundishika na wameelewa.” Alisema Kabeho
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Mhandisi Charles Francis Kabeho akizungumza na kikundi cha kupambana na dawa za kulevya shule ya sekondari Tarakea
Aidha elimu dhidi ya dawa za kulevya katika wilaya ya Rombo inaendelea kutolewa kupitia makundi mbalimbali wakimemo vijana,wanafunzi, polisi jamii, na viongozi wa dini kwa lengo la kukemea na kuondosha uuzaji,usafirishaji na utumiaji wa dawa za kulevya .
Akisoma Risala ya utii ya wananchi wa wilaya ya Rombo kwa Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk John Pombe Magufuli, Katibu Tawala (W) Abubakari Assenga amesema kuwa katika kipindi cha Januari hadi Agosti mwaka huu wilaya imefanikiwa kukamata dawa za kulevya aina ya bangi na mirungi, ambapo watuhumiwa 38 kati yao wanawake watatu walikamatwa na kufikishwa mahakamani.
Sambamba na hilo, Mhandisi Kabeho alipata fursa ya kutoa ujumbe wa Mbio Za Mwenge ambapo alisema kuwa kauli Mbiu ya Mwenge wa Uhuru mwaka huu inawakumbusha watanzania kuwekeza katika elimu, na serikali ya awamu ya tano imewekeza sana katika miundombinu ya elimu hivyo wazazi na walezi wahakikishe wanawapatia watoto mahitaji yote muhimu bila kusahau uchangiaji wa chakula shuleni.
Rombo District Council,Mkuu Bomani Street
Sanduku la Posta: P.o Box 52,Mkuu,Rombo
simu: 027-2757101
Mobile: 027-2757101
staff mail: ded@rombodc.go.tz
Copyright@2019Rombodc.all rights reserved