Wananchi wilayani Rombo wameshauriwa kutambuana na kutoa taarifa za wageni waliopo majumbani mwao pamoja na majirani zao kwa wenyeviti wa vitongoji na mabalozi, kwa ajili ya usalama wao na mali zao.
Hayo aliyasema Mkuu wa Wilaya ya Rombo Bi Agness Hokororo alipokuwa anazindua zoezi la kugawa vitambulisho vya taifa kwa wananchi katika Tarafa ya Usseri, Kata ya Kirongo Samanga .
“Hakikisha una taarifa za kutosha za jirani yako, rangi ya ngozi tu si kigezo cha utanzania,matishio ya uvunjifu wa amani yamekuwa mengi”,alisema Hokororo
Aliongeza kuwa wanaopaswa kupewa vitambulisho vya taifa ni watanzania wa kuzaliwa,kurithi na kuandikishwa na ikibainika kuna mtu asiye na sifa amepewa kitambulisho basi uongozi wote wa eneo husika utachukuliwa hatua za kisheria, kwa sababu picha zilibandikwa katika maeneo yao kwa ajili ya uhakiki na kutoa pingamizi kwa wasio na sifa.
Tunaelekea kwenye mfumo ambao ili kupata huduma za msingi lazima tutatakiwa kutambuliwa,hasa kwa tunaoishi eneo la karibu na mpaka kuna uwezekano mkubwa wa huduma nyingi za msingi kuwanufaisha watu wa nchi jirani kuliko sisi wenyewe, hivyo kila mtu aone thamani ya kitambulisho cha Taifa kilichotengenezwa kwa fedha za mlipa kodi, alimalizia Hokororo.
Naye afisa Usajili wa Vitambulisho vya Taifa (W) Bi Janeth Shayo alisema mpaka sasa asilimia 81.3 ya wananchi wa Rombo wameshasajiliwa toka zoezi lianze tarehe 10/11/2017 kwa matarajio ya kusajili wananchi wapatao 103,586 lakini ni wananchi 84,181 tu ndio wamesajiliwa.
Rombo District Council,Mkuu Bomani Street
Sanduku la Posta: P.o Box 52,Mkuu,Rombo
simu: 027-2757101
Mobile: 027-2757101
staff mail: ded@rombodc.go.tz
Copyright@2019Rombodc.all rights reserved