• Contact us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaint |
Halmashauri ya Wilaya ya Rombo
Halmashauri ya Wilaya ya Rombo

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Rombo District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • ujenzi
      • maji
      • Planning and Statitics
      • Livestock and Fishing
      • Community DEvelopment
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Elimu Msingi
      • Ellimu Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Land and natural Resources
      • Human Resource and Administration
      • Health
    • Unit
      • ICT
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Law
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
    • Organisation Structure
  • Investiment Opportunities
    • Vivutio vya utalii
    • Industry
  • Our Services
    • Water
    • Elimu
    • Watumishi
    • Kilimo
    • Health
    • Mifugo
  • Councillors
    • List of Councillors
    • Permanent Commitees
    • Scheduals of Legal sessions
  • Projects
    • Completed projects
    • Ongoing projects
    • New Project
  • Publications
    • Forms
    • Acts
    • Report
    • Taratibu
    • Taarifa za Fedha
      • Taarifa ya makisio ya Mapato
      • Taarifa ya Mapato Halisi
      • Taarifa ya Matumizi
      • MTEF
    • Guidelines
  • Media Centre
    • Videos
    • News
    • Press Releae
    • Photo Gallery
    • Speech

Tamaduni, chanzo cha ukatili wanawake,watoto

Posted on: March 7th, 2018

Picha kwa hisani ya mtandao

Tamaduni mbalimbali zinazojumuisha imani,maadili,sanaa,sheria, desturi na mila, ambazo nyingine ni za kigeni na nyingine ni za kitanzania huchangia kwa kiasi kikubwa ukatili dhidi ya wanawake na watoto,hayo yalibainishwa katika ufunguzi wa Kamati ya kupiga vita ukatili dhidi ya wanawake na watoto katika wilaya ya Rombo na mtoa mada kutoka KWIECO(shirika lisilokuwa la kiserikali linalojihusisha na kuimarisha haki za binadamu na usawa wa kijinsia) Peter Mashingia.

Mashingia alisema kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake  na watoto inaenda sambamba na kutokomeza mila na desturi kandamizi ,aliziorodhesha  baadhi ya tamaduni  hizo kuwa ni ukeketaji, mila na desturi zinazohamasishaji mimba za utotoni ,mila na desturi zinazohamasisha ndoa za lazima  mtoto kuchaguliwa mme/mke akiwa shuleni, mume kumpiga mkewe kama ishara ya upendo.

‘ Tusijadili matokeo tuangalie nini hasa sababu ya haya matukio ya ukatili kutokea , wazazi wametawaliwa sana na shughuli za uchumi  badala ya  kusimamia makuzi  ya watoto nyumbani  na wengi wanaoleta haya matatizo ukichunguza anaishi na nani utakuta anaishi na babu au bibi,hivyo tunapozungumzia mazingira salama ni budi tujihoji wenyewe’. Mkuu wa Polisi Rombo  Joseph Marwa alichangia.

Marwa aliongeza kuwa “Utamaduni wa kigeni unaathiri sana katika makuzi ya watoto kuna matukio yanatokea kwa sababu tumeruhusu sana utamaduni wa kigeni utawale maisha yetu, kuna mila  ambazo wao wanaziona ni kandamizi lakini zilitusaidia na mimba za utotoni hazikuwepo”  

Alimalizia kwa kusema kuwa, ulinzi wa jamii kwa mtoto kwa nyakati hizi ni mgumu tofauti na zamani ambapo mtoto alikuwa ni wa jamii nzima hata akikosea anaadhibiwa lakini kwa sasa  ni ngumu kwa mtu kumchapa bakora mtoto wa jirani hata kama akimuona amekosea atajisemea shauri lake na wazazi wake.

Naye afisa maendeleo ya jamii wilaya Bi Restina Mwasha alisema timu zimeundwa kuanzia ngazi ya kijiji au mtaa kwa kujumuisha wataalamu kutoka sekta mbalimbali ili kufuatilia mnyororo mzima wa matukio ya ukatili yanayotokea katika maeneo yetu na kuyaripoti eneo husika.

Aliongeza kuwa huu ni mpango wa taifa uliopewa jina la MTAKUWWA (Mpango wa Taifa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto)ambao ni mpango utakaodumu kipindi cha miaka mitano kuanzia 2018 hadi 2022 lengo likiwa ni kutokomeza ukatili wa mama na mtoto kwa asilimia hamsini hivyo ili kuifikia asilimia hii ni budi ushiriki wetu uwe wa kina na matukio yaripotiwe.

Mbali na mikakati iliyowekwa na MTAKUWWA  kamati ya ulinzi wa wanawake na watoto imeundwa kwa kufuata mwongozo ili kuboresha utoaji wa huduma kwa makundi yaliyo katika mazingira hatarishi, kwa kutoa elimu na kuhamasisha jamii kuhusu kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto, ikiwa ni pamoja na kutoa msaada wa kisheria kwa waathirika wa ukatili na kuimarisha mahusiano katika jamii.




Matangazo

  • MATOKEO YA USAHILI WA WALIOOMBA KAZI YA KUKUSANYA MAPATO NA KAZI YA USAFI August 27, 2024
  • TANGAZO LA UUZAJI WA VIWANJA VYA HALMASHAURI YA WILAYA YA ROMBO June 14, 2024
  • TANGAZO LA MNADA WA HADHARA August 26, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI YA AJIRA YA MKATABA July 16, 2024
  • View All

Habari Mpya

  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI.

    May 29, 2025
  • KARIBU KWENYE BARAZA LA MADIWANI.

    May 07, 2025
  • KARIBU KWENYE BARAZA LA MADIWANI.

    May 07, 2025
  • ZAID YA SHILINGI MILIONI MIA SITA AROBAINI NA MOJA YA KABIDHIWA KWA VIKUNDI 52

    April 17, 2025
  • View All

Videos

Maafisa Elimu Kata wakizifanyia Majaribio Pikipiki
More Videos

Kurasa za haraka

  • Muundo wa Halmashauri
  • Wasiliana Nasi Kwa
  • Miladi iliyokamilika

Kurasa za karibu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • MFUMO WA TAUSI
  • Ffars
  • Tamisemi
  • Idara ya Takwimu (NBS)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact us

    Rombo District Council,Mkuu Bomani Street

    Sanduku la Posta: P.o Box 52,Mkuu,Rombo

    simu: 027-2757101

    Mobile: 027-2757101

    staff mail: ded@rombodc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Sitemap

Copyright@2019Rombodc.all rights reserved