• Contact us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaint |
Halmashauri ya Wilaya ya Rombo
Halmashauri ya Wilaya ya Rombo

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Rombo District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • ujenzi
      • maji
      • Planning and Statitics
      • Livestock and Fishing
      • Community DEvelopment
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Elimu Msingi
      • Ellimu Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Land and natural Resources
      • Human Resource and Administration
      • Health
    • Unit
      • ICT
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Law
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
    • Organisation Structure
  • Investiment Opportunities
    • Vivutio vya utalii
    • Industry
  • Our Services
    • Water
    • Elimu
    • Watumishi
    • Kilimo
    • Health
    • Mifugo
  • Councillors
    • List of Councillors
    • Permanent Commitees
    • Scheduals of Legal sessions
  • Projects
    • Completed projects
    • Ongoing projects
    • New Project
  • Publications
    • Forms
    • Acts
    • Report
    • Taratibu
    • Taarifa za Fedha
      • Taarifa ya makisio ya Mapato
      • Taarifa ya Mapato Halisi
      • Taarifa ya Matumizi
      • MTEF
    • Guidelines
  • Media Centre
    • Videos
    • News
    • Press Releae
    • Photo Gallery
    • Speech

Shida ya Maji Rombo yaiweka Kiliwater Kitanzini

Posted on: February 6th, 2019

Baraza la madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Rombo limeazimia kuvunja mkataba baina ya Halmashauri na Kampuni ya maji ya Kiliwater inayosimamia na kuendesha miradi ya maji Rombo kwa kushindwa kumaliza tatizo la maji katika wilaya ya Rombo.

Sambamba na hilo baraza limetoa maagizo kwa Mkurugenzi Mtendaji  kuunda kamati maalumu itakayokwenda kuonana na Waziri wa maji ili kuunda mamlaka ya maji Rombo itakayokua inapata ruzuku serikalini ili kuimarisha huduma ya maji kwa wananchi.

Maamuzi hayo yamefikiwa baada ya baadhi ya madiwani kuwasilisha hoja maalum katika baraza  la madiwani lililofanyika mnamo tarehe 05.02.2019 katika ukumbi wa Halmashauri na Baraza la Madiwani kujadili hoja hiyo kwa kina.

Aidha Mhandisi wa Maji (W) John Msengi amelieleza baraza la madiwani kuwa Kampuni ya Kiliwater ipo kwa ridhaa ya warombo wenyewe baada ya serikali kujiondoa katika majukumu ya uendeshaji wa miradi ya maji moja kwa moja na kuwataka wananchi wenyewe waamue na wakaamua kuipa dhamana hiyo kampuni ya Kiliwater.

Akifafanua hilo amelieleza baraza la madiwani kuwa kabla ya mabadiliko ya sera mwaka 1995 serikali ilikuwa na majukumu makuu matatu ambayo ni sera na mipango, pili ni ujenzi wa miradi ya maji, upanuzi na ukarabati mkubwa na tatu ni uendeshaji na usimamizi  ambapo baada ya mabadiliko ya sera  Wizara iliona serikali inapata gharama kubwa kuendesha moja kwa moja na kuanzisha sera ya kuundwa vyombo huru vitakavyosaidia kusimamia na kuendesha miradi ya maji kama vile mamlaka , watu binafsi na makampuni .

Baada ya mchakato wa kuunda vyombo hivyo  kukamilika serikali ilihamisha jukumu la tatu la uendeshaji na usimamizi kwa kampuni pamoja na kuwapa  vitendea kazi, na serikali kuendelea kuisimamia Kampuni kwa utaratibu na makubaliano waliyoyaweka katika andiko .

Hata hivyo Mhe Gaston Mtuta Diwani wa Kata ya Reha ambae ndiye aliyewasilisha hoja hiyo alisema kuwa kampuni ya Kiliwater haijawahi kukaguliwa na mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (CAG), haina wafanyakazi wenye ujuzi wa kutosha na haiwajibiki kwa wananchi.

Ameongeza kuwa kampuni inazalisha maji lita za ujazo 18,000 kwa siku kipindi cha kiangazi na lita 22,000 kipindi cha masika wakati hali halisi ya mahitaji ya huduma hiyo kwa wananchi ni lita za ujazo 40,000 kwa siku hii inaonesha wazi kampuni haiwezi kumaliza tatizo la maji katika wilaya ya Rombo.

Naye Meneja wa Kiliwater (W) Prosper Kessy ameikanusha madai ya kampuni kutowajibika kwa wananchi ambapo amesema kuwa vikao vinafanyika kila mwaka na kamati za maji katika kila kijiji katika tarafa husomewa taarifa mbalimbali za utekelezaji, mipango ya kampuni pamoja na changamoto ,vyote vinawekwa wazi na wananchi wanashiriki kikamilifu.

Aidha amelihakikishia Baraza la Madiwani kuwa  Kampuni ya Kiliwater ina wataalamu wa kutosha wenye elimu kubwa na wanafanya kazi kwa weledi mkubwa. Na taarifa zote za utekelezaji wa majukumu huwasilishwa kuanzia ngazi ya  Halmashauri,mkoa  mpaka Wizara.

Kessy amesisitiza kuwa kampuni ipo kutoa huduma na sio kibiashara na kama utaratibu wa Makampuni ulivyo ni budi kukaguliwa na wakaguzi huru wa hesabu za Fedha na kutolewa taarifa , na hilo limekuwa likifanyika kwa Kampuni ya Kiliwater toka ilipoanzishwa.

Pamoja na hayo Kessy amesema ili kampuni ifanye vizuri inatakiwa kupata ushirikiano mzuri kutoka kwa wadau wote wa maji ikiwa ni pamoja na kuwa walinzi wa miundombinu ya maji na wao kama Kampuni watajitahidi kuboresha huduma ya maji kwa kutumia rasilimali walizonazo.

Matangazo

  • MATOKEO YA USAHILI WA WALIOOMBA KAZI YA KUKUSANYA MAPATO NA KAZI YA USAFI August 27, 2024
  • TANGAZO LA UUZAJI WA VIWANJA VYA HALMASHAURI YA WILAYA YA ROMBO June 14, 2024
  • TANGAZO LA MNADA WA HADHARA August 26, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI YA AJIRA YA MKATABA July 16, 2024
  • View All

Habari Mpya

  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI.

    May 29, 2025
  • KARIBU KWENYE BARAZA LA MADIWANI.

    May 07, 2025
  • KARIBU KWENYE BARAZA LA MADIWANI.

    May 07, 2025
  • ZAID YA SHILINGI MILIONI MIA SITA AROBAINI NA MOJA YA KABIDHIWA KWA VIKUNDI 52

    April 17, 2025
  • View All

Videos

Maafisa Elimu Kata wakizifanyia Majaribio Pikipiki
More Videos

Kurasa za haraka

  • Muundo wa Halmashauri
  • Wasiliana Nasi Kwa
  • Miladi iliyokamilika

Kurasa za karibu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • MFUMO WA TAUSI
  • Ffars
  • Tamisemi
  • Idara ya Takwimu (NBS)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact us

    Rombo District Council,Mkuu Bomani Street

    Sanduku la Posta: P.o Box 52,Mkuu,Rombo

    simu: 027-2757101

    Mobile: 027-2757101

    staff mail: ded@rombodc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Sitemap

Copyright@2019Rombodc.all rights reserved