• Contact us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaint |
Halmashauri ya Wilaya ya Rombo
Halmashauri ya Wilaya ya Rombo

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Rombo District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • ujenzi
      • maji
      • Planning and Statitics
      • Livestock and Fishing
      • Community DEvelopment
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Elimu Msingi
      • Ellimu Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Land and natural Resources
      • Human Resource and Administration
      • Health
    • Unit
      • ICT
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Law
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
    • Organisation Structure
  • Investiment Opportunities
    • Vivutio vya utalii
    • Industry
  • Our Services
    • Water
    • Elimu
    • Watumishi
    • Kilimo
    • Health
    • Mifugo
  • Councillors
    • List of Councillors
    • Permanent Commitees
    • Scheduals of Legal sessions
  • Projects
    • Completed projects
    • Ongoing projects
    • New Project
  • Publications
    • Forms
    • Acts
    • Report
    • Taratibu
    • Taarifa za Fedha
      • Taarifa ya makisio ya Mapato
      • Taarifa ya Mapato Halisi
      • Taarifa ya Matumizi
      • MTEF
    • Guidelines
  • Media Centre
    • Videos
    • News
    • Press Releae
    • Photo Gallery
    • Speech

Rombo yatoa mkopo wa milioni 61.5 kwa vikundi 20

Posted on: January 10th, 2020

Halmashauri ya wilaya ya Rombo imetoa mkopo wa shilingi milioni 61.5  kwa  jumla ya vikundi  20, vya wanawake (12), Vijana ( 7) na wenye ulemavu ( 1), kupitia  10%(asilimia kumi) ya mapato ya ndani ,ambayo kwa mujibu wa sheria ni lazima  iende  kwenye makundi hayo ili kuyainua kiuchumi.

Afisa Maendeleo ya Jamii (W) Patricia Kinyange  ameeleza kuwa vikundi vilivyokuwa vimeomba mkopo vilikuwa 55 vilivyokuwa na thamani ya milioni 275  lakini  kutokana na mapato madogo ya Halmashauri  kamati ya wilaya ilikaa na kuchuja angalau kila Kata ipate kikundi kimoja na baada ya mchujo vilipatikana vikundi 20 ambavyo ndivyo vinavyopokea mkopo huo.

Ameongeza kuwa mikopo hii inayotolewa sasa ni ya kipindi cha robo ya kwanza kwa mwaka wa fedha  2019/2020,  na hivi karibuni  halmashauri inategemea  kumalizia kutoa mikopo kwa  robo ya pili.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Rombo Mhe. Agness Hokororo  amevitaka vikundi vilivyopata mkopo kufanya biashara zao kwa kufuata sheria na taratibu huku wakijifunza kutunza akiba zao zitakazowasaidia kufanya uzalishaji mkubwa zaidi,  ili nia njema ya serikali ya kuwainua wananchi kiuchumi ionekane .

Sambamba na hilo  amewaasa  wanavikundi kujiepusha na biashara za magendo,  na  kuweka wazi iwapo wakijihusisha, serikali itawakamata na fedha yote ya kikundi itapotea na kuwasababishia hasara na kushindwa kufanya marejesho kitu kitakachopelekea Halmashauri kuwashitaki mahakamani.

“Natamani vikundi hivi viendelee kiuchumi na baadae hata kuungana na kuwa na mtaji mkubwa zaidi ili kuanzisha viwanda vitakavyokuwa vinatengeneza  bidhaa zilizoongezwa thamani  na bidhaa za uzalishaji ambazo zitakuwa zinatoka Rombo,” amezungumza Godwin Chacha ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Rombo.

Kabla ya kupewa mikopo hiyo vikundi hivyo vilipata mafunzo ya siku mbili juu ya uandaaji wa vitabu vya fedha vinavyotunza kumbukumbu, Elimu ya ujasiriamali,usimamizi wa akaunti , hatua za kuchukua kabla ya kuchukua mkopo, namna ya kufanya marejesho na jinsi ya kujisajili PPRA.


Matangazo

  • MATOKEO YA USAHILI WA WALIOOMBA KAZI YA KUKUSANYA MAPATO NA KAZI YA USAFI August 27, 2024
  • TANGAZO LA UUZAJI WA VIWANJA VYA HALMASHAURI YA WILAYA YA ROMBO June 14, 2024
  • TANGAZO LA MNADA WA HADHARA August 26, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI YA AJIRA YA MKATABA July 16, 2024
  • View All

Habari Mpya

  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI.

    May 29, 2025
  • KARIBU KWENYE BARAZA LA MADIWANI.

    May 07, 2025
  • KARIBU KWENYE BARAZA LA MADIWANI.

    May 07, 2025
  • ZAID YA SHILINGI MILIONI MIA SITA AROBAINI NA MOJA YA KABIDHIWA KWA VIKUNDI 52

    April 17, 2025
  • View All

Videos

Maafisa Elimu Kata wakizifanyia Majaribio Pikipiki
More Videos

Kurasa za haraka

  • Muundo wa Halmashauri
  • Wasiliana Nasi Kwa
  • Miladi iliyokamilika

Kurasa za karibu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • MFUMO WA TAUSI
  • Ffars
  • Tamisemi
  • Idara ya Takwimu (NBS)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact us

    Rombo District Council,Mkuu Bomani Street

    Sanduku la Posta: P.o Box 52,Mkuu,Rombo

    simu: 027-2757101

    Mobile: 027-2757101

    staff mail: ded@rombodc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Sitemap

Copyright@2019Rombodc.all rights reserved