• Contact us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaint |
Halmashauri ya Wilaya ya Rombo
Halmashauri ya Wilaya ya Rombo

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Rombo District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • ujenzi
      • maji
      • Planning and Statitics
      • Livestock and Fishing
      • Community DEvelopment
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Elimu Msingi
      • Ellimu Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Land and natural Resources
      • Human Resource and Administration
      • Health
    • Unit
      • ICT
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Law
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
    • Organisation Structure
  • Investiment Opportunities
    • Vivutio vya utalii
    • Industry
  • Our Services
    • Water
    • Elimu
    • Watumishi
    • Kilimo
    • Health
    • Mifugo
  • Councillors
    • List of Councillors
    • Permanent Commitees
    • Scheduals of Legal sessions
  • Projects
    • Completed projects
    • Ongoing projects
    • New Project
  • Publications
    • Forms
    • Acts
    • Report
    • Taratibu
    • Taarifa za Fedha
      • Taarifa ya makisio ya Mapato
      • Taarifa ya Mapato Halisi
      • Taarifa ya Matumizi
      • MTEF
    • Guidelines
  • Media Centre
    • Videos
    • News
    • Press Releae
    • Photo Gallery
    • Speech

Rombo yajipanga kupunguza utapiamlo

Posted on: November 23rd, 2020

Katika harakati za kupambana na athari za utapiamlo na kuboresha hali ya lishe katika wilaya ya Rombo, kamati ya lishe wilaya  chini ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri, imejipanga kutoa elimu ya kutosha kwa wananchi wote kuhakikisha athari za utapiamlo zinapungua.

Akizungumza mara baada ya kufungua kikao cha kamati ya lishe wilaya, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri  ya Wilaya ya Rombo Ndugu Chrispin Mng’anya amesema kuwa ni vyema elimu ya lishe itolewe kwa wamama wanaonyonyesha na  wajawazito ili watoto wanapozaliwa wawe tayari mama zao wanaelewa umuhimu wa lishe bora kwa watoto.

“Siku elfu moja(1000) za mwanzo za maisha ya mtoto ni msingi wa lishe bora kwa mtoto na lishe isipozingatiwa katika muda huo inaathiri ukuaji wa mtoto kimwili na kiakili”, alisema Mng’anya.

Aliongeza kuwa agenda ya lishe iwe ya kudumu kwenye vikao vinavyofanyika katika maeneo yetu ikiwa ni pamoja na uwepo wa timu maalum katika kila ngazi itakayosaidiana na Afisa Lishe kutoa elimu ya lishe kwa jamii.

Naye Mganga Mkuu wa Wilaya, Bw. Boaz Mwaikugile amesema kuwa kutokuwa na mpangilio mzuri wa chakula na lishe kwa ujumla kunaweza kusababisha maradhi mengi katika mwili wa binadamu likiwepo tatizo la utapiamlo.

“Magonjwa mengi yanayowapata binadamu yana uhusiano mkubwa sana na suala la lishe, mbali na tatizo la utapiamlo kuna maradhi kama vile kisukari, shinikizo la damu na mengine mengi”alisema Mwaikugile

Naye Mhandisi wa maji(W) Bw John Msengi ambaye ni mjumbe wa kamati hiyo ameshauri kabla ya kamati kuanza kazi rasmi ya kupambana na utapiamlo ni vema kufanya uchunguzi na kutambua ukubwa wa tatizo la utapiamlo kiwilaya na takwimu zioneshe maeneo yenye shida zaidi ili nguvu kubwa ielekezwe katika maeneo hayo.

Hali ya utapiamlo inasababishwa na ukosefu wa lishe/chakula bora pamoja na maambukizi ya mara kwa mara yanayosababisha mtu kukosa hamu ya kula na kushindwa kula mlo kamili. Wakina mama wajawazito na wanaonyonyesha wapo kwenye hatari zaidi ya ya kupata utapiamlo na watoto wadogo wanaweza kuathirika toka tumboni iwapo mama hakupata lishe bora kabla na wakati wa ujauzito.




Matangazo

  • MATOKEO YA USAHILI WA WALIOOMBA KAZI YA KUKUSANYA MAPATO NA KAZI YA USAFI August 27, 2024
  • TANGAZO LA UUZAJI WA VIWANJA VYA HALMASHAURI YA WILAYA YA ROMBO June 14, 2024
  • TANGAZO LA MNADA WA HADHARA August 26, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI YA AJIRA YA MKATABA July 16, 2024
  • View All

Habari Mpya

  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI.

    May 29, 2025
  • KARIBU KWENYE BARAZA LA MADIWANI.

    May 07, 2025
  • KARIBU KWENYE BARAZA LA MADIWANI.

    May 07, 2025
  • ZAID YA SHILINGI MILIONI MIA SITA AROBAINI NA MOJA YA KABIDHIWA KWA VIKUNDI 52

    April 17, 2025
  • View All

Videos

Maafisa Elimu Kata wakizifanyia Majaribio Pikipiki
More Videos

Kurasa za haraka

  • Muundo wa Halmashauri
  • Wasiliana Nasi Kwa
  • Miladi iliyokamilika

Kurasa za karibu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • MFUMO WA TAUSI
  • Ffars
  • Tamisemi
  • Idara ya Takwimu (NBS)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact us

    Rombo District Council,Mkuu Bomani Street

    Sanduku la Posta: P.o Box 52,Mkuu,Rombo

    simu: 027-2757101

    Mobile: 027-2757101

    staff mail: ded@rombodc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Sitemap

Copyright@2019Rombodc.all rights reserved