• Contact us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaint |
Halmashauri ya Wilaya ya Rombo
Halmashauri ya Wilaya ya Rombo

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Rombo District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • ujenzi
      • maji
      • Planning and Statitics
      • Livestock and Fishing
      • Community DEvelopment
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Elimu Msingi
      • Ellimu Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Land and natural Resources
      • Human Resource and Administration
      • Health
    • Unit
      • ICT
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Law
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
    • Organisation Structure
  • Investiment Opportunities
    • Vivutio vya utalii
    • Industry
  • Our Services
    • Water
    • Elimu
    • Watumishi
    • Kilimo
    • Health
    • Mifugo
  • Councillors
    • List of Councillors
    • Permanent Commitees
    • Scheduals of Legal sessions
  • Projects
    • Completed projects
    • Ongoing projects
    • New Project
  • Publications
    • Forms
    • Acts
    • Report
    • Taratibu
    • Taarifa za Fedha
      • Taarifa ya makisio ya Mapato
      • Taarifa ya Mapato Halisi
      • Taarifa ya Matumizi
      • MTEF
    • Guidelines
  • Media Centre
    • Videos
    • News
    • Press Releae
    • Photo Gallery
    • Speech

ROMBO MSAKO WA NYUMBA HADI NYUMBA, HATUA KALI ZA KISHERIA KUCHUKULIWA KWA ATAKAEKUTWA NA MTOTO WA SHULE NYUMBANI.

Posted on: January 16th, 2024

Mkuu wa Wilaya ya Rombo, mkoani Kilimanjaro, Raymond Mwangwala amewataka wazazi wote wenye watoto wa umri wa kuanza shule, kuhakikisha wanawaandikisha na kwamba kwa wale ambao watakiuka hilo, watachukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kushtakiwa.

Mwangwala ametoa rai hiyo leo jumatatu, januari 15,2024 baada ya kufanya ukaguzi katika baadhi ya shule ikiwemo shule ya Msingi ubaa ili kuangalia hali ya uandikishaji wa wanafunzi wa darasa la awali na darasa la kwanza

"Wanafunzi wameweza kujitokeza kwa wingi kujiandikisha darasa la kwanza na awali, zipo shule ambazo zimevuka malengo ikiwemo shule ya Msingi Ubaa ambayo maoteo kwa darasa la awali ilikuwa ni wanafunzi 22 lakini mpaka sasa wameandikishwa 60 lakini darasa la kwanza wanafunzi waliopaswa kuandikishwa ni 30 lakini tayari wameandikishwa 40".

Aidha mkuu huyo amesema tayari wameanza msako wa nyumba kwa nyumba na hata kwenye magulio na Masoko ili kuhakikisha watoto wote wenye umri wa kwenda shule wanakwenda  ili kutimiza haki zao za kimsingi za kupata elimu.

"Kwa sasa viongozi kuanzia ngazi za vitongoji, Kata, Tarafa na Hata Wilaya, wameanza kuzunguka kuanzia kwenye vitongoji nyumba kwa nyumba wakiongozwa na mimi kiongozi wao kuhakikisha watoto wote wanaopaswa kupelekwa  shule, wanapelekwa"

"Tutachukua hatua kali za kisheria ikiwemo kuwashitaki wazazi ambao hawatawapeleka watoto shule ili hali umri wa kwenda shule umefika. Mtoto kupata elimu ni haki ya msingi ya binadamu hivyo tutachukua hatua kwa yeyote ambaye atakiuka haki hii ya msingi".

Mkuu huyo ametoa pia wito kwa jamii, kuwaripoti watoto wote wenye umri wa kwenda shule ambao wanazurura mitaani au wameachwa nyumbani ili hatua zichukuliwe kwa wazazi.

Ametumia pia nafasi hiyo kuwataka walimu kutimiza wajibu wao wa kuwafundisha wanafunzi ili kuwawezesha kupata elimu bora kama ilivyokusudiwa.

Mpaka kufikia Januari 11,2024 katika Wilaya hiyo tayari wameandikisha wanafunzi 4,639 wa awali na wanafunzi 4,454 wa darasa la kwa kwanza ikiwa ni asilimia 90 ya malengo yaliyowekwa.

KUONA VIDEO BOFYA LINK HAPA CHINI.

https://youtu.be/jQbMyyKPRKo?si=ep9IQm-p4i9ht4B2

Matangazo

  • MATOKEO YA USAHILI WA WALIOOMBA KAZI YA KUKUSANYA MAPATO NA KAZI YA USAFI August 27, 2024
  • TANGAZO LA UUZAJI WA VIWANJA VYA HALMASHAURI YA WILAYA YA ROMBO June 14, 2024
  • TANGAZO LA MNADA WA HADHARA August 26, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI YA AJIRA YA MKATABA July 16, 2024
  • View All

Habari Mpya

  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI.

    May 29, 2025
  • KARIBU KWENYE BARAZA LA MADIWANI.

    May 07, 2025
  • KARIBU KWENYE BARAZA LA MADIWANI.

    May 07, 2025
  • ZAID YA SHILINGI MILIONI MIA SITA AROBAINI NA MOJA YA KABIDHIWA KWA VIKUNDI 52

    April 17, 2025
  • View All

Videos

Maafisa Elimu Kata wakizifanyia Majaribio Pikipiki
More Videos

Kurasa za haraka

  • Muundo wa Halmashauri
  • Wasiliana Nasi Kwa
  • Miladi iliyokamilika

Kurasa za karibu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • MFUMO WA TAUSI
  • Ffars
  • Tamisemi
  • Idara ya Takwimu (NBS)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact us

    Rombo District Council,Mkuu Bomani Street

    Sanduku la Posta: P.o Box 52,Mkuu,Rombo

    simu: 027-2757101

    Mobile: 027-2757101

    staff mail: ded@rombodc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Sitemap

Copyright@2019Rombodc.all rights reserved