Mkuu wa wilaya ya Rombo Mh.Raymond Mwangwala amefanya mkutano na Wananchi wa Kata ya Mahida Wilayani Rombo Mkoani Kilimanjaro kwa Lengo la kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi wa eneo Hilo.
Katika mkutano huo pia Mkuu wa Wilaya ya Rombo ametumia nafasi hiyo kuhimiza Wananchi kujitokeza kwa wingi katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 27, 2024 na pia kushiriki katika zoezi la kujiandikisha kwa wapiga kura litakalofanyika kuanzia tarehe 11-20 Oktoba 2024,
Aidha Mh.Mwangwala amewataka wananchi kuchukua tahadhari na kuwa makini na ugonjwa wa MPOX ambao upo nchi za jirani huku akisisitiza na kuwataka Madaktari kupeleka semina hasa kwa Wananchi wanaokaa maeneo ya Pembezoni mwa Nchi jirani
Rombo District Council,Mkuu Bomani Street
Sanduku la Posta: P.o Box 52,Mkuu,Rombo
simu: 027-2757101
Mobile: 027-2757101
staff mail: ded@rombodc.go.tz
Copyright@2019Rombodc.all rights reserved