Mkuu wa Wilaya ya Rombo Mhe. Raymond Steven Mwangwala tarehe April 22, 2024 amefanya mkutano wa hadhara wenye lengo la kusikiliza na kutatua kero za wananchi wa Tarafa ya Mengwe.
Katika mkutano huo uliofanyika holili katika viwanja vya ofisi za mtendaji wa kata Mhe. Mwangwala aliambatana na kamati ya ulinzi na usalama, Wataalamu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Rombo na wengine kutoka Taasisi zinazowahudumia wananchi kwa ukaribu ikiwemo Wakala wa Barabara za Vijijini na Mji (TARURA) , Wataalamu kutoka Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira (rombowasa) pamoja na wataalamu kutoka Shirika la Umeme Tanzania ( TANESCO).
Katika kusikiliza kero za wananchi wa Tarafa Ya Mengwe kata ya holili , Mkuu wa wilaya alipokea changamoto mbalimbali zikiwemo zinazohusu Elimu, Miundombinu ya barabara, Maji, Umeme, Afya, migogoro mbalimbali ya Ardhi na changamoto za Kisheria zinazowakabili wananchi hao.
Mkuu wa Wilaya akishirikiana na wataalamu aliongozana nao walifanikiwa kutolea majibu kwa baadhi ya changamoto huku nyingine zikipaa utatuzi wa papo kwa papo na nyingine zilipokelewa kwa maelekezo ya kupatiwa mwarobaini wake.
Hatahivyo, Dc Mwangwala amewataka viongozi wa TARURA kurekebisha miundombinu ya barabara hasa maeneo yenye uhitaji zaidi kutokana na uharibifu ulosababishwa na mvua zilizonyesha.
Sambamba na hilo Dc Mwangwala amesema suala la Usalama katika Wilaya sio jukumu la polisi peke yake bali ni jukumu la kila mwananchi, hivyo amewataka wananchi kuwa mstari wa mbele katika kutoa ushirikiano endapo uhalifu utatokea ili kusaidia kutunza amani na usalama hasa maeneo hayo ambayo yapo mpakani na nchi jirani ya Kenya.
Naye Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Rombo amemuhakikishia Mkuu wa Wilaya kutatua kero kwa wakati
“Tutahakikisha kero hizi tunazitatua kwa wakati bila kuathiri maeneo mengine kwani Wataalamu wetu tumewaelekeza kufuatilia maeneo yote yenye kero na kushughulikia kwa wakati hususani eneo la elimu, Ustawi wa Jamii, Maendeleo ya Jamii pamoja na eneo la sheria hivyo nipende kutoa shukrani zangu kwa Mkuu wa Wilaya kwa ziara hii ya kutatua kero na nikuhakikishie tumejipanga kuondoa kero za wananchi kwa ajili ya kukuza uchumi wao.”
Rombo District Council,Mkuu Bomani Street
Sanduku la Posta: P.o Box 52,Mkuu,Rombo
simu: 027-2757101
Mobile: 027-2757101
staff mail: ded@rombodc.go.tz
Copyright@2019Rombodc.all rights reserved