“Serikali inaweka alama katika mpaka wa kimataifa kati ya Kenya naTanzania na kujenga barabara zitakazosaidia kufanya patrol, kudhibiti magonjwa ya kuambukiza ya wanadamu na mifugo, utoroshaji wa mifugo pamoja na wahamiaji haramu”.
Hayo aliyasema Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo Ya Makazi Mh, William Lukuvi akiwa katika ziara ya siku moja wilayani Rombo.
Aliongeza kuwa kwa kufanya hivyo serikali itakuwa inakamilisha agizo la umoja wa nchi za Africa ambalo limeagiza mipaka yote ya kimataifa iliyowekwa na wakoloni kuimarishwa pamoja na andiko kusainiwa na Maraisi wa pande zote mbili za mipaka hiyo.
Aidha Waziri Lukuvi ameagiza watanzania wote waliojenga ndani ya eneo huru la mpaka wa kimataifa waondolewe sambamba na wakenya waliojenga katika eneo hilo kwa upande wa Tanzania bila kusubiri tamko la Maraisi.
Naye Mkuu Wa Wilaya Ya Rombo Bi Agness Hokororo akitoa taarifa ya wilaya kwa upande wa Ardhi alisema changamoto kubwa ni kutokuwepo kwa Baraza la Ardhi la wilaya na umuhimu wake kutokana na asilimia sitini(60) ya malalamiko ni migogoro ya Ardhi.
Wilaya ya Rombo ina mpaka wa kimataifa na Kenya wenye umbali kwa kilometa zipatazo 100, alama za mpaka zipo katika hali nzuri kwa upande wa mfungamano wake( alama moja hadi nyingine) huku 8 zikihitaji kujengwa upya,6 hazifikiki kwa uraisi,alama 21 zimemomonyoka na kukatika na zinahitaji marekebisho.
Rombo District Council,Mkuu Bomani Street
Sanduku la Posta: P.o Box 52,Mkuu,Rombo
simu: 027-2757101
Mobile: 027-2757101
staff mail: ded@rombodc.go.tz
Copyright@2019Rombodc.all rights reserved