• Contact us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaint |
Halmashauri ya Wilaya ya Rombo
Halmashauri ya Wilaya ya Rombo

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Rombo District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • ujenzi
      • maji
      • Planning and Statitics
      • Livestock and Fishing
      • Community DEvelopment
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Elimu Msingi
      • Ellimu Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Land and natural Resources
      • Human Resource and Administration
      • Health
    • Unit
      • ICT
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Law
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
    • Organisation Structure
  • Investiment Opportunities
    • Vivutio vya utalii
    • Industry
  • Our Services
    • Water
    • Elimu
    • Watumishi
    • Kilimo
    • Health
    • Mifugo
  • Councillors
    • List of Councillors
    • Permanent Commitees
    • Scheduals of Legal sessions
  • Projects
    • Completed projects
    • Ongoing projects
    • New Project
  • Publications
    • Forms
    • Acts
    • Report
    • Taratibu
    • Taarifa za Fedha
      • Taarifa ya makisio ya Mapato
      • Taarifa ya Mapato Halisi
      • Taarifa ya Matumizi
      • MTEF
    • Guidelines
  • Media Centre
    • Videos
    • News
    • Press Releae
    • Photo Gallery
    • Speech

Mikopo bila riba yawanufaisha Vijana 401

Posted on: June 17th, 2019

Kiasi cha shilingi Milioni 138.6 zawanufaisha Vijana 401 wilayani Rombo kupitia mfuko wa  maendeleo  ya wanawake, vijana na walemavu ambao unatokana na  asilimia kumi (10%)  ya mapato ya ndani ambapo  4% ni ya wanawake, 4% ya Vijana na 2% ya walemavu.

Hayo ameyasema Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Rombo Ndugu Magreth L John alipokuwa akitoa taarifa kwa wajumbe kutoka ofisi ya Waziri Mkuu ambao ni Maafisa Maendeleo ya Vijana walipozuru wilayani  Rombo leo tarehe 17.6.2019 ili kukagua asilimia nne (4%) ya mapato ya ndani ambayo Halmashauri inatakiwa kukopesha vikundi vya vijana bila riba.

Ndugu Magreth ameeleza kuwa kwa mwaka wa fedha 2016/17 kiasi cha shilingi 10,600,000.00 zilitolewa kwa vikundi saba vyenye jumla ya watu 88, mwaka wa fedha2017/18 kiasi cha shilingi 46,500,000.00 kilitolewa kwa vikundi 22 vyenye jumla ya watu 217,na mwaka wa fedha 2018/19  kiasi cha shilingi 49,500,000.00 kimeshatolewa kwa vikundi 12 vyenye watu 96.

Ameongeza kuna vikundi vingi vya vijana vinaendelea kuwezeshwa kwa awamu kulingana na hali ya makusanyo na uwepo wa fedha, sambamba na hilo Halmashauri ya wilaya kupitia idara ya Maendeleo ya Jamii imeendelea kutoa elimu ya mikopo na ujasiriamali kwa kuwazungukia vijana vijijini.

Akizungumzia mafanikio yaliyoonekana ni pamoja na kufanikiwa kulipa deni la mkopo wa Wizara kiasi cha shilingi milioni 16, na kupokea fedha ya marejesho kiasi cha shilingi milioni 32 ambazo nazo zimekopeshwa vikundi vya vijana

Aidha changamoto kubwa ni vijana kujiunga kwenye vikundi ili wapate mikopo lakini wakishapata wanasambaratika na kugawana fedha hivyo ili Halmashauri ipate marejesho imebidi Halmashauri ishughulike na wadhamini wao kwa sababu kila kikundi inabidi kiwe na wadhamini hivyo wao ndio wanaobanwa ili tupate marejesho.

Naye Ndugu Godfrey Nyaisa ambaye ni Afisa Maendeleo ya Vijana kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana  ,Ajira na walemavu aalisifia jitihada zinazofanywa na Halmashauri kwa kuhakikisha Vijana wanakopeshwa kupitia 4% na inaonekana kweli vijana wanachapa kazi kulingana na kasi yao ya marejesho.

Nchi inatengenezwa na vijana ambao ndio nguvu kazi kubwa na ndio wanategemewa waweze kusaidia azma ya taifa kufikia uchumi wa kati ifikapo 2025,hivyo ni budi halmashauri kuendelea kuhamasisha vijana kujiunga katika vikundi na kuanzisha viwanda vidogo vidogo.

"Lengo la serikali ni kutaka vijana wawezeshwe ili waweze kujiajiri , na tumefurahishwa kusikia vijana wamemaliza deni lao la mkopo wa Wizara kwasababu katika halmashauri nyingi nchini kumekuwa na changamoto sana kwenye urejeshaji wa mikopo kuna maeneo mengine madeni ni makubwa na waliokopa hawajulikani walipo na wengine hawatambuliki", ameyasema haya Ndugu Amina Sanga  Afisa Maendeleo ya Vijana kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana  ,Ajira na walemavu.                                                    

Matangazo

  • MATOKEO YA USAHILI WA WALIOOMBA KAZI YA KUKUSANYA MAPATO NA KAZI YA USAFI August 27, 2024
  • TANGAZO LA UUZAJI WA VIWANJA VYA HALMASHAURI YA WILAYA YA ROMBO June 14, 2024
  • TANGAZO LA MNADA WA HADHARA August 26, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI YA AJIRA YA MKATABA July 16, 2024
  • View All

Habari Mpya

  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI.

    May 29, 2025
  • KARIBU KWENYE BARAZA LA MADIWANI.

    May 07, 2025
  • KARIBU KWENYE BARAZA LA MADIWANI.

    May 07, 2025
  • ZAID YA SHILINGI MILIONI MIA SITA AROBAINI NA MOJA YA KABIDHIWA KWA VIKUNDI 52

    April 17, 2025
  • View All

Videos

Maafisa Elimu Kata wakizifanyia Majaribio Pikipiki
More Videos

Kurasa za haraka

  • Muundo wa Halmashauri
  • Wasiliana Nasi Kwa
  • Miladi iliyokamilika

Kurasa za karibu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • MFUMO WA TAUSI
  • Ffars
  • Tamisemi
  • Idara ya Takwimu (NBS)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact us

    Rombo District Council,Mkuu Bomani Street

    Sanduku la Posta: P.o Box 52,Mkuu,Rombo

    simu: 027-2757101

    Mobile: 027-2757101

    staff mail: ded@rombodc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Sitemap

Copyright@2019Rombodc.all rights reserved