Mhe. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan katika ziara yake wilayani Rombo leo tarehe 9.11.2018 ametoa rai kwa watumishi wa umma kuwa na ushirikiano ndani ya serikali, chama tawala na serikali pamoja na jamii kwa ujumla.
Ameongeza kuwa katika harakati za kuwaletea wananchi maendeleo ni budi watumishi wa umma kufanya kazi kwa ushirikiano, uadilifu, weledi na uaminifu mkubwa kwa kila mmoja kwenye nafasi yake kuhakikisha anawajibika ipasavyo.
"Nimetumwa na Mhe.Rais niwaambie mshirikiane, kama hamtaki kupendana msipendane,lakini katika kazi shirikianeni kwasababu wote tunajenga nyumba moja inayoitwa Tanzania kwa itikadi zozote tulizonazo bado tunatawaliwa na sheria moja, miongozo na kanuni za serikali".alisema Mama Samia
Aidha amesisitiza kuwepo kwa uhusiano mzuri kati ya watumishi wa umma na jamii pamoja na kauli nzuri kwa wananchi pasipo kutumia mabavu.
Hata hivyo aliipongeza wilaya ya Rombo kwa maendeleo yaliyopatikana katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa awamu ya tano ya Mhe Rais John Pombe Magufuli ikiwa ni pamoja na kudumisha amani na utulivu.
Rombo District Council,Mkuu Bomani Street
Sanduku la Posta: P.o Box 52,Mkuu,Rombo
simu: 027-2757101
Mobile: 027-2757101
staff mail: ded@rombodc.go.tz
Copyright@2019Rombodc.all rights reserved