Kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Rombo Mwl. CHsrles Mganga amehitimisha mafunzo ya mfumo wa FFARS kwa watendaji wa kata na vijiji na kuomba watendaji hao kuweza kuyazingatia mafunzo hayo waliyoyapata na endapo watakumbana na changamoto yoyote wasisite kuwasiliana na ofisi ya IT na uhasibu ili kutatua changamoto hizo.
Mwl. Mganga alito ushauri kwa watendaji hao wakati akifunga mafunzo hayo yaliyofanyika kwa siku nne katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri.
Hata hivyo, aliyekuwa mkufunzi mkuu kutoka Ofisi ya Mhasibu wa Wilaya Ndg. Adolf Anyisile maeeleza kuwa, mafunzo hayo yatakuwa na tija kubwa katika kuhakikisha uwepo na upatikanaji wa taarifa sahihi za matumizi ya fedha kwa ngazi za kata na vijiji.
“mafunzo haya yataendana na kasi ya maendeleo ya sayansi na teknolojia kwa kutoka kataika mfumo wa kizamani (manual),” aliongeza Anyisile.
Rombo District Council,Mkuu Bomani Street
Sanduku la Posta: P.o Box 52,Mkuu,Rombo
simu: 027-2757101
Mobile: 027-2757101
staff mail: ded@rombodc.go.tz
Copyright@2019Rombodc.all rights reserved