Wanawake wa Halamashauri ya Wilaya ya Rombo wameungana kwa pamoja na kuwatembelea wafungwa katika gereza la Rombo na kuwakabidhi vitu mbalimbali ikiwemo maboksi ya sabuni za vipande, mifuko ya sabuni za unga pamoja na vingine vingi ikiwa ni kuonesha matendo ya huruma katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani ambayo kwa wilaya ya Rombo yamefanyika leo tarehe 07 machi 2024.
Hatahivyo waliungana na mgeni rasmi Mhe. Raymond Mwangwala ambaye pia ni ndiye Mkuu wa Wilaya ya Rombo kwa sasa katika kukabidhi vitu hivyo katika Gereza hilo.
Rombo District Council,Mkuu Bomani Street
Sanduku la Posta: P.o Box 52,Mkuu,Rombo
simu: 027-2757101
Mobile: 027-2757101
staff mail: ded@rombodc.go.tz
Copyright@2019Rombodc.all rights reserved