Mkurugenzi Mtendaji wilaya ya Rombo Bi Magreth John ameiomba jamii nzima ya Rombo kumlinda mtoto wa kike dhidi ya mimba za utotoni ili aweze kutimiza ndoto zake, hayo aliyazungumza katika mkutano wa kuhamasisha shughuli za maendeleo katika kata ya Motamburu Kitendeni.
Bi Magreth alisisitiza elimu juu ya mimba kwa wanafunzi wa kike ni muhimu kutolewa kuanzia ngazi ya familia ,ni wajibu wa wazazi wote wawili kuhakikisha wanakaa na binti zao kuwaambia ukweli bila kificho kuhusu mabadiliko ya ukuaji na madhara ya mahusiano na jinsia tofauti kabla ya wakati, kwasababu mtoto anapopata mimba shuleni anakwamisha ndoto zake na ndoto za wazazi walizokuwa nazo kwa binti yao.
Aliongeza kuwa watoto wa kike wanakutana na vishawishi vingi ambavyo baadae vinawaingiza katika matatizo ya kupata ujauzito wakiwa shuleni kitu kinachosababisha kukatisha masomo yao na kuwaharibia muelekeo wa maisha, lakini wahusika wanaowafanyia unyama huu ni vijana na watu wazima katika maeneo yetu.
“Vijana tuwajali watoto wa kike kama dada zetu/wadogo zetu tuwalinde, na hili sio kwa vijana hata wazee mnawaharibu mabinti wanaosoma” Alisema Bi Magreth.
Wilaya ya Rombo ni miongoni za Wilaya zenye kiwango kikubwa cha wanafunzi wa kike kupata mimba mashuleni , kitu ambacho kinasababisha kukatisha masomo yao na kuingia katika umama katika umri mdogo , hivyo elimu ya ukuaji na mimba ni muhimu kutolewa kuanzia ngazi ya familia na jamii nzima iwe mlinzi wa mtoto wa kike , kila mtu amuangalie mtoto wa kike kama mwanaye, dada, mjukuu na mtu anaehitaji ulinzi wa jamii nzima.
Rombo District Council,Mkuu Bomani Street
Sanduku la Posta: P.o Box 52,Mkuu,Rombo
simu: 027-2757101
Mobile: 027-2757101
staff mail: ded@rombodc.go.tz
Copyright@2019Rombodc.all rights reserved